CHADEMA waache kutumia neno Kamanda bila sifa stahiki

CHADEMA waache kutumia neno Kamanda bila sifa stahiki

Kuna mambo makubwa ya kuwekea nguvu na muda kuliko kukasirishwa na vitu vidogo kama hivyo. Watu wanajiita majina mbalimbali kwa sababu zao iwe ni kwa mzaha, kiasili, kidini, kichawi au hata chapa yao binafsi. Kama Harmonize anajiita jeshi na Lady Jaydee komando, halina madhara kwa mtu mwingine. Lakini CHADEMA ni chama ambacho kinawakilisha na kugusa maisha ya watu wengi moja kwa moja hivyo ni lazima wajitafakari na kujiita majina yenye maana nayanayo wakilisha sifa ya jamii wanayoiongoza.
Wao wengi wameona wajiite makamanda,wewe mmoja unataka wajiitaje ili uridhike?
 
Kwahiyo ww na hiyo fake id ya kizungu na picha ya mzungu ndio ww? Au ukweli ni nini kwako?
Muhimu ni maudhui na ujumbe unaotolewa, si sura au jina. Kuweka mkazo kwenye vitu vidogo vidogo kama hivi kunapoteza maana halisi ya mazungumzo yenye tija. Lazima ujue kutofautisha kati ya vitu vya mhusika na wahusika.
 
Msivyo na akili hamkawii kusema neno hilo linachochea uvunjifu wa amani.
Nani kasema linachochoe uvunjufu wa amani? Shida neno lenyewe halina uhalisia na vitendo vyao.
 
Muhimu ni maudhui na ujumbe unaotolewa, si sura au jina. Kuweka mkazo kwenye vitu vidogo vidogo kama hivi kunapoteza maana halisi ya mazungumzo yenye tija. Lazima ujue kutofautisha kati ya vitu vya mhusika na wahusika.
Unakosoa wenzako, wakati ww mwenyewe umechemka.
 
Wao wengi wameona wajiite makamanda,wewe mmoja unataka wajiitaje ili uridhike?
Sina haja ya kuridhika, lakini kusolewa ni jambo la msingi. Hata mimi nakubali kukosolewa, kwa maana Dunia imefika hapa ilipo kwa sababu ya opinion za watu mbalimbali, hatuwezi wote tukawa na opinion moja. Penye kasoro ni vyema kutoa kasoro ili mtu au watu wajiulize na wajisahihishe ni wap pako vizuri na ni wap panapohitaji marekebisho.
 
Huwezi chambua hoja bila kujua mrengo wa mleta hoja.
umesskia watu wanaokwambia MAMA HADAIWI KITU, huko jimboni hakuna madawa, walimu, ajira, umeme, barabara, huyo mtu ukimchungiza ni MBOGAMBOGA, kwanini mnajificha kwenye mwavuli wa "sina chama" wakati una kadi ya kijani?
😂😂😂😂😂😂😂
 
Habari,

Nimekuwa kimya kwa miaka mingi, kutokana na miangaiko ya hapa na pale.
Lakini kila ninapopita mitaani, vichochoroni na kwenye madimbwi ya maji na kutana na neno hili 'KAMANDA" nikirudi kwenye Uso kitabu, X, Insta, nikienda JF nakutana na neno hili "KAMANDA". Yaani mtu hata chakula chake cha siku kinamshinda anajiita ''KAMANDA''. Kiujumla KAMANDA ni neno kubwa sana na lenye uzito sana, nikisema hivi, nafikiri wale Makamanda wenzangu wa Jeshi wananielewa. Hili neno kiujumla Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanalitumia kimkakati na wameshindwa kulitendea haki.

Basi Kamanda ni nani? neno "Kamanda" kwa ujumla linahusiana na uongozi, mamlaka, na uwezo wa kusimamia au kuongoza katika nyanja mbalimbali, hasa za kijeshi, usalama, na hata harakati za kijamii, katika hali yoyote ile ya mvua au jua na kuwa na msimamo wa kujitoa mhanga kwa ajili ya wenzako au misimamo yako.

Unaweza kuwa "umekula mbuzi mzima lakini mkia umekushinda", hapa kwenye kujitoa "mhanga", mseme tu ukweli na muwe-honest na nafsi zenu kumewashinda, hivyo nasema hivi "CHADEMA acheni kujipa vyeo vya movie za action, wakati hata kujificha msituni kwa siku moja kunawashinda!"

:Tssk:
Kasome tena kiswahili!
 
Back
Top Bottom