CHADEMA: Waandishi wazuiliwa kuingia Mahakamani kesi ya Lissu

CHADEMA: Waandishi wazuiliwa kuingia Mahakamani kesi ya Lissu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema waandishi wa habari wamezuiwa kuingia katika ukumbi wa Mahakama Kuu kuripoti mwenendo wa kesi inayohusu vikwazo vya kumwona Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, akiwa mahabusu.

PICHA za Matukio ya Leo Julai 03, 2026 za Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEM.jpg

Taarifa hiyo imetolewa kupitia ukurasa rasmi wa chama mtandaoni, ikieleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya Lissu kutoa wito kwa umma kukichangia chama pamoja na kuwaomba waandishi kufuatilia na kuripoti mwenendo wa shauri hilo.

1784713438568.png

​
Fuatilia mwenendo wa Kesi: Kesi ya Lissu: Bwana Jela wa Ukonga, Andrew Ntamamiro akifanyiwa dodoso na Tundu Lissu

Shauri hilo linalohusu vikwazo vya kumwona Lissu katika Gereza la Ukonga limeendelea kusikilizwa Julai 22, 2026 katika Mahakama Kuu, Masjala ya Dar es Salaam. Kesi hiyo inahusisha madai ya ukiukwaji wa haki ya faragha pamoja na madai ya kutosikilizwa kwa mazungumzo ya siri kati ya mawakili na mteja wao wakati wa ziara gerezani.

Katika mwenendo wa shauri hilo, Mkuu wa Gereza la Ukonga, Andrew Ntamamiro, alitoa ushahidi kama shahidi wa upande wa wajibu maombi katika shauri la kikatiba lililofunguliwa na mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo. Kesi hiyo inaendelea kufuatiliwa kutokana na uzito wa hoja zinazohusu haki za watuhumiwa na upatikanaji wa haki ndani ya mfumo wa sheria.

​
 
Ni vizuri kutumia mambo mengine kutafuta kiki au public sympathy ndugu zangu na sio upotoshaji useless kama huo,

wanazuiwaje wakati vitu viko live?🐒
 
Kama Kiongozi wako ndio uyu Tundu Lissu pole tu👈

mana yule tayali kaanza kuugua ukichaa
yumkin Damu za watoto wa masikini zinafanya kazi✍️
Wewe ndio think tank wa CCM. Aahaha aaaha aaah aaaha
 
Back
Top Bottom