CHADEMA waje na ajenda gani kwenye mkutano wao wa kwanza baada ya kutoka kifungoni?

CHADEMA waje na ajenda gani kwenye mkutano wao wa kwanza baada ya kutoka kifungoni?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kama ilivyosemwa kwamba chama hiki kikubwa kabisa cha upinzani hapa nchini kitaanza mikutano yake ya hadhara hivi karibuni, kutokana na hali ya mambo ilivyo Kwa sasa na mabadiliko makubwa ya kisiasa yaliyotokea baina ya utawala wa kikwete magufuli na hatimae Samia, ni hoja zipi unadhani zitaleta mvuto Kwa wananchi?

1. Pongezi Kwa mama Kwa kuruhusu mikutano ya wapinzani?

2. kulaani ukopaji na ukuaji wa deni la taifa?

3. Kusoma lisala ya kumponda na kumshutumu hayati?

4. Kupanda Kwa gharama ya maisha na namna ambavyo ilani yao ingedhibiti hiyo hali?

5. Kukosekana Kwa ajira Kwa vijana.?

Au una dhani ni hoja zipi zitaleta mvuto sana Kwa raia wa kawaida?
 
Ajenda ya Chadema ni moja tu, nayo ni KUIMARISHA CHAMA CHAO
 
Ajenda gan bwana wee wakati watakuwa wakiandaliwa cha kusema na yule chair wao aliyelamba upawa wa asali[emoji23] kwa niaba ya sir'hundred.

Hakuna jipya zaid ya kulalamikia tume huru ya uchaguzi, katiba na haki ya wao kuzungumza, mazungumzo yenyewe yatakuwa yaliyochujwa kutoka kwa chairperson wa chama.

Wakithubutu kuleta mboyoyo utaona Wakishughulikiwa kitaalamu
 
1 na 3.
1. Wampongeze na kummwagia sifa zote rais Samia kwa kuruhusu mikutano ya kisiasa.

3. Isiwe risala tu, kila atakayepanda jukwaani ainange serikali ya awamu ya 5, ambayo Samia alikuwa makamu wa Rais, na kuipaka kila aina ya matope (kupanda kwa gharama za maisha, mgao wa umeme/maji/madawa/chakula, nk).

Wakizungumzia hayo watauteka mji wote! Yani wasizungumzie kitu kingine chochote zaidi ya kumponda Hayati Magufuli.

Top up iwe kufagilia ushoga.

Btw, chadema wenyewe wana ajenda au hoja gani za maana ambazo watu hawajazisikia?
 
Katiba Mpya: UGATUZI kwa kiingereza Devolution!
 
Kama ilivyosemwa kwamba chama hiki kikubwa kabisa cha upinzani hapa nchini kitaanza mikutano yake ya hadhara hivi karibuni, kutokana na hali...
Ajenda namba 1 ya chadema ni kulamba asali ajenda namba 2 ni kupambana na marehemu hizi ndiyo ajenda kuu za chadema
 
Mambo ya kusema ni mengi sana utawara huu wajikite kwenye taarifa nyeti za ufisadi , rushwa ,ajira na upandaji wa gharama za maisha, I'm sure wata win umma wasije na propaganda zile zile za kila siku hii ni karata yao ya mwisho kisiasa kuaminika kwamba ni wapinzani na sio walamba asali kama tunavyoambiwa na wanachama wa chama cha mambuzi [emoji1][emoji1]
 
Bado kujadili hali ya kiuchumi jinsi inazidi kuwa mbaya nchini tunajadili masuala ya vyama jamii forum zaman kulikuwa na watu wasomi lkn siku hizi wameingia watu wa ovyoo
 
Nadhani ajenda ya kwanza kwa nini wabunge wa COVID ni michepuko au wake wa viongozi wakuu wa Chadema, wakiwa majukwaani wanawashambulia, wakirudi na mishahara toka Bungeni, wananunua chakula, wanakaa mezani na familia zao wanaila.

Huu ndio unafiki plusPlus
 
Unajua kwenye ishu ya KATIBA mpya na tume huru ni kama mama amesha wawahi labda kama wataongelea kukazia tu.

..jambo la msingi ni katiba iwe bora, pia tume iwe huru.

..na vyote viwili vipatikane ndani ya muda unaotarajiwa.

..kwamba nani kamuwahi mwenzake sidhani kama ni jambo muhimu.
 
Back
Top Bottom