CHADEMA waje na mfumo wa 'Primaries'

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
20,189
Reaction score
29,663
Nashauri chama changu cha CHADEMA waje na mfumo wa Primaries, kwenye Uchaguzi wa kumpata mgombea Urais wa chama 2025. Tena mchakato uanze 2024. Kama wanavyofanya Marekani, hii itaongeza demokrasia kwenye chama na pia wagombea kujitangaza kwa uwazi.

Kura zitapigwa kimkoa au kikanda kulingana na resources. Wanachama wote wa CHADEMA wenye kadi ya uanacha wataruhusiwa kupiga kura kumchagua mgombea urais.

Hii itasaidia kuongeza coverage ya chama. Nakumbuka wakati Mh Mbowe anagombea Urais , mfumo wa Primaries ulitumika kumchagua. Kura zilipigwa kwa Kanda.

Hivyo turudishe huu mfumo, na mkutano mkuu ufanyike mwisho wa Primaries ili kumuidhisha aliyepata kura nyingi kwenye primaries za chama.

Long live CHADEMA, chama cha Watanzania.
 
Naunga mkono hoja. Kitu kama hiki nami niliwahi washauri Chadema https://www.jamiiforums.com/threads...zitto-nani-anaujua-msimamo-wa-dr-slaa.297451/
P
 
wazo limepokelewa
 
Mgombea awe mdude
 
Watuletee na walimu wa kutufundisha Sekondari. Mitihani migumu sekondari. Tunashindwa kuing'oa CCM
 
Wazo zuri Sana hili, huu mfumo unaepusha kama yale yaliyotokea mwaka 2015.

Tindo brazaj JokaKuu
 
Wazo zuri Sana hili, huu mfumo unaepusha kama yale yaliyotokea mwaka 2015.

Tindo brazaj JokaKuu

Naunga mkono hoja, hili ni wazo sahihi. Na mtu yoyote anayetaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya CDM, wangalau awe ametumikia au kuwa mwanacdm hai sio chini ya miaka mitano, na awe alikuwa analipa ada zote za uanachama. Hii itaepusha watu wanaotumia udhaifu wa uongozi, kuja kuchukua nafasi za watu wenye moyo na chama.
 

Nakubaliana nawe ila miaka 5 ni mingi mno. Kumbuka "ukiteka kifaru cha adui kulikoni kutokukitumia?" -- JPM.

Tujifunze Kwa wenzetu Kenya pia.

WasIofaa kwenye primaries hawawezi kutoboa.
 
Nafikiri Mdude anafaa kuwa mwenyekiti wa chama taifa, afu hapo kwenye uraisi apewe Sugu.
Mkuu usidharau watu upepo wa siasa huwa ni wa ajabu,Rais Reagan wa USA alikuwaga muigizaji,Rais wa Indonesia wa sasa alikuwa shoe shine,Rais wa Uturuki Erdigan alikuwa mcheza mpira,Rais wa India alikuwa muuza chain.
Orodha ni ndefu,Politics haina mwenyewe ni upepo.

By the way kama Mwinyi,Kikwete na Magufuli wameweza hao watashindwa nini?
 

Hili ni wazo bora kabisa ambalo ni muhimu likazingatiwa.

Kwa mustakabala mpana wa nchi tupiganie pia fursa za kuwa coalitions za vyama kama za Jubilee, NASA, Azimio au Kenya.

Tupanue wigo wa demokrasia tutapiga hatua kama nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…