CHADEMA waje na mfumo wa 'Primaries'

CHADEMA waje na mfumo wa 'Primaries'

Proved Tindo asinyanyapaliwe awaye yote anayekidhi vigezo vya kuwa mwanachama kwa mujibu wa katiba.

Primaries kama zilivyo zitoe fursa sawa kwa kila mwanachama kugombea nafasi yoyote chamani kwa mujibu wa katiba.

Kusifungamanishwe strings zingine zisizokuwapo.

Kwa hakika wasiofaa hawatatoboa bali wakomavu.
 
Mgombea awe mdude

Mapendekezo ni primaries ambapo anayekidhi kigezo cha uanachama anayo fursa.

Mdude kama wanachama wengine atagombea kama anataka na atachaguliwa na wanachama kama watakavyoona na atakavyowashawishi.

Kwani umeona tuko kwenye kupendekeza majina ya wagombea hapa ewe chawa wa Mama?
 
Mapendekezo ni primaries ambapo anayekidhi kigezo cha uanachama anayo fursa.

Mdude kama wanachama wengine atagombea kama anataka na atachaguliwa na wanachama kama watakavyoona na atakavyowashawishi.

Kwani umeona tuko kwenye kupendekeza majina ya wagombea hapa ewe chawa wa Mama?
🤣🤣🤣Chawa kazini
 
Ulichokileta ni sahihi hasa ukisomwa kwa haraka haraka, unaonekana umewahusisha wanachama kwenye kushiriki kumchagua mgombea wao wa Urais..

Lakini tukubaliane, mazingira na muda ni kitu kikubwa kinachoweza kuathiri jina la mgombea atakayepitishwa, tumeshaona matukio yanavyoweza kuongeza nguvu ya mgombea au kumpunguzia umaarufu.

Mfano Lissu 2020, tukio lililompata lilichangia kwa kiasi kikubwa kukuza umaarufu wake, na hasa muda uliokuwa umebaki kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa 2020..

Hapa ni muhimu kufanyia utafiti wa kutosha muda utakaotumika kupiga kura ili kumpata mgombea, ili isijekutokea kura zikapigwa akashinda mgombea fulani, halafu baada ya muda fulani tukielekea kwenye uchaguzi, litokee tukio litakalopunguza nguvu na umaarufu wa mgombea husika, kama usipokuwepo umakini wa kutosha kwenye hilo, basi kuna dalili ya siku moja kuumbuka..

Au...

Itakuwa vipi pale ambapo baada ya kumpata mgombea wa chama, akajiunga chamani mtu mwingine atakayekuwa na nguvu na umaarufu zaidi ya mgombea aliyechaguliwa na wanachama, watakataa kumpa hiyo nafasi hata kama jamii ya watanzania itaonekana kumkubali?

Hapa mfano wa Lowassa unaingia moja kwa moja, hata kama wengine wakipuuza kwa sababu nyepesi, lakini ni ukweli kwamba, impact ya Lowassa kujiunga Chadema imeacha historia, na imeweka rekodi, hasa kuzingatia idadi ya.kura alizopata, na kuongeza wabunge majimboni.

Umaarufu wa chama pekee hapa hauwezi kuwa sababu inayojitosheleza, ni ubinafsi na kujikweza tu; kwani tumeshaona uhalisia chama kikiwa na wagombea wake, na kufanya siasa miaka mitano, lakini bado walishindwa kufikia idadi ya kura alizovuna Lowassa akiwemo Dr. Slaa 2010 tena mbele ya JK aliyeonekana kuwa dhaifu kwa wakati ule..

The truth is, kwenye haya mambo kuna factors huwa zinaingiliana, kuzikataa ni sawa na kuukataa ukweli, kujidanganya, hivyo kubaki kujidumaza tu kuyafikia maendeleo ya chama, kwani idadi ya kura za mgombea urais huchangia ruzuku..
 
Ahsante kwa kuunga wazo,lakini kwa kuwa wewe ni kada wa CCM kwa nn usiwape wazo hili chama chako ili kuondokana na kuchapisha fomu moja kabla ya kuwa na mahaba na Chadema. CCM hawashauriki etiii
CCM tayari wana system ya uongozi in place, grooming of future leaders inafanyika by now tayari tunajua baada ya Samia anakuja nani, na sio kama usultani wenu!.
P
 
Back
Top Bottom