Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Bara John Heche amesema chama hicho kina kila hoja za kushindana na chama cha mapinduzi na watazitumia pindi wakianza kufanya ziara na kuzungumza na wananchi.
Heche amesema hayo leo akiwa jijini Arusha na kueleza kuwa miongoni mwa hoja walizonazo ni juu ya uwepo wa ubadhirifu kwenye mradi wa reli ya treni iendayo haraka(SGR).
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Heche amedai mchakato wa kutangaza zabuni na mshindi kupatikana kutokufanyika kiusahihi lakini pia gharama zilizotumika zina mashaka pamoja na kutokuwa na ubora unaohitajika kwa mabehewa yanayotumika katika treni hizo.