Pre GE2025 CHADEMA wajipanga kuanika madudu ya SGR, wanusa harufu ya wizi na ufisadi

Pre GE2025 CHADEMA wajipanga kuanika madudu ya SGR, wanusa harufu ya wizi na ufisadi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi kweli ile treni ya mwendo kasi, inayoitwa Royal express inarudisha gharama kweli? au kama zilivyo ndege hata wakisafiri watu 50 kwenye EMU yenye mabehewa 8 yote sawa tu?
Bado najiuliza, yale mabehewa ya ghorofa, yatakuwa na reli yake tofauti na hizi reli mbili zilizopo sasa au itajengwa reli nyingine?
Nawaza kwa kuweweseka tu.....Kumaanisha!!. 🤔 😳
 
CCM ni vibaka - tutasimama na Lissu & Heche.

Hawa wajinga laza tuwaonyeshe adabu. Pigo la.kwanza hakuna mjinga hata mmoja atapanga folenikuchagua eti kiongozi October hii
 
kukosa agenda na kufilisika hoja ni kitu mbaya sana, hasa kwa mtu mwenye stress za kufilisika na anae ugulia athari za kubeti na kuliwa pension yake yote ya ubunge,

muhindi sio mtu mzuri,
kubeti ni kitu mbaya sana aise, jamaa mpaka kazeeka 🐒
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Bara John Heche amesema chama hicho kina kila hoja za kushindana na chama cha mapinduzi na watazitumia pindi wakianza kufanya ziara na kuzungumza na wananchi.

Heche amesema hayo leo akiwa jijini Arusha na kueleza kuwa miongoni mwa hoja walizonazo ni juu ya uwepo wa ubadhirifu kwenye mradi wa reli ya treni iendayo haraka(SGR).

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Heche amedai mchakato wa kutangaza zabuni na mshindi kupatikana kutokufanyika kiusahihi lakini pia gharama zilizotumika zina mashaka pamoja na kutokuwa na ubora unaohitajika kwa mabehewa yanayotumika katika treni hizo.

Yani wewe una upofu wa itikadi.

Nyau de adriz
 
Hivi kweli ile treni ya mwendo kasi, inayoitwa Royal express inarudisha gharama kweli? au kama zilivyo ndege hata wakisafiri watu 50 kwenye EMU yenye mabehewa 8 yote sawa tu?
Bado najiuliza, yale mabehewa ya ghorofa, yatakuwa na reli yake tofauti na hizi reli mbili zilizopo sasa au itajengwa reli nyingine?
Nawaza kwa kuweweseka tu.....Kumaanisha!!. 🤔 😳
Huwa inapita unakuta behewa zima wamekaa wawili tu mtu na mpenzi wake
 
Bado najiuliza, yale mabehewa ya ghorofa, yatakuwa na reli yake tofauti na hizi reli mbili zilizopo sasa au itajengwa reli nyingine?
Wameleta mabehewa ya ghorofa?
 
Yes nchi ilipoa sana aisee, tunataka amsha amsha kama hizi tupunguze kusikiliza yanga na simba na manara wao 24/7
Ma Mc kwenye harusi utasikia piga kelele Kwa wana Yanga halafu tena unasikia piga kelele kwa wana Simba...na juzi kati Amos Makala nae tarehe 5 kwenye sherehe za CCM hivyo hivyo na bungeni upuuzi ulele na redio zote zimetapakaa wahuni wanaitwa wachambuzi wa soka. Huku bank kuu yetu na hazina vimegeuzwa kama vibanda vya M-pesa nikujichotea tu mahela anapewa Abdul
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche amesema kuwa chama hicho kipo katika mchakato wa kuanika Nyaraka zote za Ununuzi wa Mabehewa ya Treni ya Mwendokasi (SGR) adai kuna wizi wa kutupwa ulifanyika.
View attachment 3244431
Japokuwa mimi siyo Chadema lakini sikuwahi kuacha kumuelewa Heche, jamaa ni mwamba kweli kweli tangu akiwa mwenyekiti wa bavicha taifa achana na pambalu ambaye hakuwa na impact yoyote
 
Pamoja na haya yote bado kuna watu ukipita huko ukiwasikia wanavyosifia, hakika wabongo ni wacongo version 2
 
Huwa inapita unakuta behewa zima wamekaa wawili tu mtu na mpenzi wake
Nimeshuhudia hilo juzi, kwa makusudi nilikata tiketi ya Royal express ya saa 12 jioni kutoka Dom. Mabehewa mengi yalikuwa matupu, halafu ilitanguliwa na Express nyingine kwa saa moja tu....Sijui hapa kama TRC wanafanya kweli biashara au ni kampeni za kisasa. 🤔
 
Kwamba Wana habari nyeti na nzito nzito za hujuma ya SGR, Lakini wanasubiri Ziara zianje ndio wakaseme!!
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Bara John Heche amesema chama hicho kina kila hoja za kushindana na chama cha mapinduzi na watazitumia pindi wakianza kufanya ziara na kuzungumza na wananchi.

Heche amesema hayo leo akiwa jijini Arusha na kueleza kuwa miongoni mwa hoja walizonazo ni juu ya uwepo wa ubadhirifu kwenye mradi wa reli ya treni iendayo haraka(SGR).

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Heche amedai mchakato wa kutangaza zabuni na mshindi kupatikana kutokufanyika kiusahihi lakini pia gharama zilizotumika zina mashaka pamoja na kutokuwa na ubora unaohitajika kwa mabehewa yanayotumika katika treni hizo.
Kama wanataka kufanya siasa na kudumu kwenye siasa waachane na SGR na bwawa la umeme watajiharibia Kwa watanzania wao labda wakosoe jinsi inavyoendeshwa au usimamizi la sivyo watachukiwa na watanzania au wakosoe tanesco kukatakata umeme licha ya bwawa kukamilika ila ujenzi itawacosti big time
 
Hivi huyu anajuwa kuna tender ya commercial na technical? anadhani tender inaamuliwa kwa bei tu? ziko tender zinabeba uzito 80% commercial na 20 mengine na ziko 70% Technical sio commercial. Kila tender inatumwa sehemu mbili Tech na Commercial kwa maana hiyo sio bei inaamua kila kitu.
 
Back
Top Bottom