CHADEMA wakija kukubali huu upumbavu ndo utakuwa mwisho wao

CHADEMA wakija kukubali huu upumbavu ndo utakuwa mwisho wao

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,439
Reaction score
145,410
1. Samia ni muuaji. Hakuna aliyemchagua awe Rais. Yeye na hilo genge lake analotawala nalo ni haramu. Nchimbi naye alikuwa haramu. Ndejembi naye ni haramu.

Kwa sasa nchi haina uongozi ulio halali na uliopewa ridhaa ya kuongoza na wananchi.

Watu wanaomuita huyo Samia ‘Rais’ wanakera sana na ni wapumbavu wasiojielewa.

Mbaya zaidi, licha ya kuua maelfu ya watu, wakiwemo watoto wengi, kuna watu bado wanamuita huyo Samia eti ‘mama’.

Mnamuitaje ‘mama’ mtu aliyeua watu wengi hivyo?

Huyo Samia alikuwa anaitwa hivyo affectionately. Hiyo affection ilikwisha Oktoba 29, 2025.

Mtamuitaje ‘mama’ mtu aliyeua watoto? Mna akili timamu kweli nyie watu?

CHADEMA mkija kuanza kumtambua huyo muuaji na kuanza kumuita ‘mama’, mtatupoteza watu wa kawaida kama mimi ambao hatuna vyama ila tunaongozwa na kanuni.

Watu kama mimi tumeamua kuwaunga mkono kwa sababu tumeona walau kwa juu juu, kidogo mnawajali Watanzania, hususan wale wqsio na chochote kama wale watoto waliouliwa na Samia.

Sasa fanyeni huo upumbavu wa kumtambua Samia na kuanza kumuita hilo jina la upendo halafu muone tutavyowatosa.

2. Hakuna kufanya maridhiano na Samia na CCM yake.

Mridhiane na Samia kwa misingi gani?

Tayari CCM walishawachezea akili kwenye yale maridhiano mliyotaka kufanya nao kipindi kile cha Kinana na Mbowe.

CCM hawana nia ya kweli ya kuridhiana nanyi.

Wanachokitaka ni uhalali feki kwa nyinyi kuwatambua wao.

Nanyi msiwe wapumbavu wa kutumika kama chambo tu.

Maridhiano na wauaji ni usaliti mkubwa sana kwa wale watoto waliomwaga damu zao ili Samia aendelee kung’ang’ania madarakani.

Kamwe hamtasameheka mkija kufanya huo ushenzi.

You’ve been warned…….respectfully.

Kwa nini walimuua huyu mtoto?

IMG_8639.jpeg
 
Hakuna Maridhiani na wauaji..

Ili hayo maridhiano yafanyike yafuatayo lazima yafanyike
1. Waliohusika wote na mauaji, yani aliyetoa amri ya kuua mpaka yule aliyevuta trigger risassi ikatoka na kuua wawajibishwe.
2. Maiti za Watangayike zipatike ili wazikwe kwa heshima kama wanadamu.. wale si ng'ombe
3. Uchaguzi mkuu urudiwe.
4. Katiba mpya
5. Maridhiano

Kinyume na hapo hakuna Maridhiano ...kamwe kamwe..
 
Orodha ya Wanasiasa waliohama Kutoka CHADEMA.
1. Freeman Mbowe.
2. Wilbroad Silaha.
3.Kitila mkumbo.
4. Patrobas Katambi.
5. David Silinde
6. Joshua Nassari.
7. COVID 19.
8. Wilfred Lwakatare.
9. Mabere Marando.
10. Abdalah Safari.
 
CHADEMA imeshavurugika Mkuu.
Kuna Mambo mengi sana yameivuruga Taasisi, Chadema imebaki jina tu.

FEDHA CHAFU ILIINGIZWA CHADEMA NDIO IKAWA MWISHO WA TAASISI.
Misukosuko ya hapa na pale huwa haikosekani.

Chama kilichovurugika kwa uhakika ni CCM.

CCM wametapakaa damu za watoto wa Kitanzania kama huyu…..

IMG_8639.jpeg


Huyu mtoto hata jina lake hatulijui.

Hatujui alizikwa wqpi.

Samia hata kutoa pole kwa wazazi na ndugu wa huyu mtoto, hajawahi.

Hii ndo kazi ya kutukuka iliyofanywa na polisi wa CCM.

Hivi kweli mtu unaweza kujenga hoja kwamba CCM wako sawa?
 
💯%.

Na dhamiri inawasumbua sana na ndo maana unawaona wanahaha kutafuta maridhiano ili wapate uhalali licha ya “kushinda kwa kuchaguliwa” na watu milioni 31 kati ya milioni 32 “waliojitokeza kupiga kura”.
Wanataka maridhiano na Chadema kwasababu wanajua sasa hivi Watanganyika wote wapo nyuma(bega kwa bega) na Chadema.. Hivyo wanafanya kila mbinu ili waridhiane na CDm.. Maana wakifanikiwa kuridhiana na CDM basi wanachi watakuwa wapole...... Mauaji ya Oct 29 ni laana ambayo haitakaa ifutike milele.. zile damu bado zinalia ardhini.... Na hazitanyamaza mpaka Haki ipatikane na Tanganyika mpya izaliwe
 
Hakuna Maridhiani na wauaji..

Ili hayo maridhiano yafanyike yafuatayo lazima yafanyike
1. Waliohusika wote na mauaji, yani aliyetoa amri ya kuua mpaka yule aliyevuta trigger risassi ikatoka na kuua wawajibishwe.
2. Maiti za Watangayike zipatike ili wazikwe kwa heshima kama wanadamu.. wale si ng'ombe
3. Uchaguzi mkuu urudiwe.
4. Katiba mpya
5. Maridhiano

Kinyume na hapo hakuna Maridhiano ...kamwe kamwe..
💯%.
 
CHADEMA imeshavurugika Mkuu.
Kuna Mambo mengi sana yameivuruga Taasisi, Chadema imebaki jina tu.

FEDHA CHAFU ILIINGIZWA CHADEMA NDIO IKAWA MWISHO WA TAASISI.
Hizo ni ndoto, CHADEMA ya sasa ni imara mara mia zaidi ya CHADEMA iliyokuwa chini ya uongozi wa Mbowe. Kuhaha huku kwa CCM kunadhihirisha hayo, kitendo cha Lissu kuwa na strict principles ndiyo kimezidi kuiimarisha CHADEMA na ndipo CCM wanahangaika na wale wenye price tag ndani ya CHADEMA.
 
Hebu rudini nchini kwanza tusaidiane kuing'oa CCm.
Sio nyie mnabeba mabox huko USA mnaingiza dolari halafu sisi tunaumiziwa ndugu zetu huku nyie mkituhamasisha tu.
Njooni nyumbani tupambane kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom