CHADEMA wakubali yaishe majimbo baada ya serikali tatu kukubalika katiba mpya

CHADEMA wakubali yaishe majimbo baada ya serikali tatu kukubalika katiba mpya

CCM hawawezi kukubali wananchi wenyewe wasimamie raslimali zao. Wanataka mapato yote yaendelee kupelekwa Dar es salaam ili yawanufaishe wao na familia zao. Wanatoa visingizio kwamba: "Suala hilo litatugawa". Ajabu na kweli! Wananchi kusimamia raslimali ni marufuku kwa kuwa watagawanyika!!! Sijui iwapo watanzania wana mang'amuzi ya kutosha kwa jambo hili.

images

Mbaya zaidi kwa CCM ni rasimu ya katiba mpya msajiri wa vyama vya siasa amepata automatic knock out.
 
USA wamefanikiwa kimaendeleo kwa Kuwa na serikari za majimbo kwani inampa nafasi Rais kutawala kwa ufanisi na kwa Gharama nafuu zaidi ya serikari tatu ambazo Hakuna mfano wa kuigwa ambapo serikari 3 zimefanikiwa kimaendeleo. Ni bora Mara kumi wangeiga muungano wa UK ambapo serikari zinaongozwa na mawaziri wakuu au wangefanya kama Ujerumani mashariki na magharibi walivyoungana na Kuwa kitu kimoja hata China na hong cong Ifanyike jitihada zenji na Bara tuwe kitu kimoja na Kuwa na Serikari Moja tu inatosha sisi ni ndugu moja Hakuna lisilowezekana .kumbuka muungano upo ktk wizara 4 tu hivyo Serikari tatu Ina Maana serikari ya shirikisho itakuwa na wizara Nne tu hapo lazima kutaleta mkanganyiko
 
Maoni ya tume juu ya serikali ya majimbo ni DHAIFU na ya WOGA! GHARAMA wanazosema za uendeshaji hazilingani na gharama za mikoa na wilaya!

wameona mbali coz hapo watu kama hawa wanaoanza kutangaza jamhuri zao watapata nguvu.kila kanda itakuwa shaghalabaghala yaani huyu madini hayatoki yule gesi haitoki mwingine samaki hawatoki n.k n.k na sehemu zisizo na rasilimali nyingi zitabaki chini.hatimaye chuki zitaanza na tutaangaliana kwa kanda tunazotoka,dharau/ufahari/kutambiana na mambo kama hayo yatakua kutugawa.
 
Kuna mengi katika rasimu hii ya katiba yanayotia moyo mojawapo ni kwamba:
Mchakacho wa kupata tume ya uchaguzi, hali kadhalika tume hiyo iwe ndiyo yenye mamlaka katika usajili wa vyama vya siasa badala ya Tendwa ambayo ame-hang mahali pasipoeleweka.
Na chakusikitisha ni kuwa bado wajumbe watalazimika kuidhinishwa/kupendekezwa na rais,kama ccm itakuwa madarakani basi maana yake ni kuwa wajumbe watalazimika kupata ridhaa toka kwa mwenyekiti wa ccm(Rais)hapo bado kuna ukakasi
 
Kwa muungano wa serikali tatu,naona dalili za uwezekano wa Zanzibar kujiondoa kwa kasi zinanukia.
 
Serikari za majimbo zinapaswa ziwe mbili tu yaani Zenji na Bara kwani wimbi la majimbo litaleta gharama kubwa kuongoza Kama ilivyo kwa serikari tatu .wananchi hawajapata uelewa wa kutosha juu utawala wa Majimbo na siku wakijua vizuri watazitambua Faida zake
 
wameona mbali coz hapo watu kama hawa wanaoanza kutangaza jamhuri zao watapata nguvu.kila kanda itakuwa shaghalabaghala yaani huyu madini hayatoki yule gesi haitoki mwingine samaki hawatoki n.k n.k na sehemu zisizo na rasilimali nyingi zitabaki chini.hatimaye chuki zitaanza na tutaangaliana kwa kanda tunazotoka,dharau/ufahari/kutambiana na mambo kama hayo yatakua kutugawa.

Majimbo yanatakiwa yawe Mawili tu sio zaidi yaani ZNZ atawale Gavana na Tz Bara yote atawale Gavana aishi pale magogoni Rais awe Mmoja tu na ahamie Dodoma hiyo ni serikari nafuu kuliko serikari tatu ambapo ni gharama kuiendesha
 
Wapenda urais kazi kwenu serikali 3 zote ukose@Six,maembe,mamvi,at al

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hivi kati ya maoni haya ya rasimu yepi yalikuwa maoni ya CCM? nahitaji kujua hilo! Maana naona maoni karibia yote ni mwiba kwa CCM!
 
Kwa muungano wa serikali tatu,naona dalili za uwezekano wa Zanzibar kujiondoa kwa kasi zinanukia.

Chezea zenji wewe wao wana nyimbo na bendera Yao tayari wanasubiri serikari 3 wapate mwanya wa kusepa .dawa ya kuepuka migongano ni kuungana Kama ujerumani walivyoungana na Kuwa wamoja na Kuwa na serikari moja tu
 
Dah! Sasa mambo 7 ya muungano ndio yawe na mawaziri 15???

Ni dhahiri wajumbe wa Zanzibar waloko kwenye hii tume wamefanya kazi nzuri zaidi ya wale wa Bara..................mtazamo tu
 
Bunge la CCM hawawezi ipitisha rasimu hii iwe katiba!
Vipengele vilivyonifurahisha:
Serikali 3
Mawaziri wasizidi 15 na wasiwe wabunge
Wakuu wa Wilaya wajadiliwe kwenye serikali ya Zanzibar na ya Tanganyika
Deni la Taifa sasa liwe ndani ya katiba
KILICHO NIHUZUNISHA:
Rasimu haija dhibiti safari za Rais maana JK anachokifanya anaweza akaja Rais mwingine akaiga haya mambo;Safari karibia 400 nje ya nchi ndani ya miaka 8 ni mzigo sana kwa tax payers!
Yani wewe katika fikra zako zako zote safari za rais umeona ni bonge la ishu kweli ubinadamu kazi.
 
Suala la majimbo ni ubaguzi tu wala hayana msingi wowote zaidi ya kuimarisha ukanda,ukabila na udini.
 
Kitendo cha rais kupewa mamlaka ya kutia mkono kwenye tume ya uchaguzi nadhani inakosa sifa ya kuwa huru na haki maana sidhani kama rais ataniteua ni mwenyekiti alafu nione kwenye uchaguzi anapoteza nikubali, nitachakachua ili na mimi nipate kulinda wadhifa wangu
 
Hadi hapo tulipofika ni hatua nzuri na kwakweli binafsi nampongeza JK na wajumbe wa tume hiyo kuna mwanga unajitokeza. Kuna mambo mengi ya msingi yamependekezwa sasa kwenye hatua zinazofuata hayo mambo mazuri yasichakachuliwe hili si suala la CCM wala CDM ni wa Tanzania wote. Kuhusu sera ya majimbo bado CDM waendelee nayo kama mfumo wao kichama na hii itakuwa inawapa elimu watu namna mfumo huu ulivyo na manufaa.
 
Serikali za Majimbo ndiyo njia effective .Ni kwa vipi ichochee ukabila?
 
Nachelea kusema huenda CDM wasije pata angalau mbunge mmoja wa muungano maana sijuwi km watapita kwenye mtego huu. Haya yangu macho
 
Yani wewe katika fikra zako zako zote safari za rais umeona ni bonge la ishu kweli ubinadamu kazi.

Nchi zenye akili zililiona hilo na kuliwekea udhibiti,safari karibia 400 sasa za JK ndani ya miaka 8 tu zimetumaliza sana bila tija yyt ile!

USA kwa mfano,Rais anaomba hela kwenye Congress na hajiamulii tu safari!Tanzania tunaweza fanya hivyo!
 
Serikali za Majimbo ndiyo njia effective .Ni kwa vipi ichochee ukabila?

Technically Mzee Wariona hajakataza serikali za majimbo bali amewaachia WATZ wenyewe waamue kwenye serikali yao ya Tanganyika lkn akakataa lisiwepo kwenye serikali ya Muungano!

CHADEMA endeleeni na mchakato wa serikali za majimbo ili iwemo kwenye rasimu ya serikali ya Tanganyika!
 
Back
Top Bottom