CHADEMA wakubali yaishe majimbo baada ya serikali tatu kukubalika katiba mpya

Hivi kati ya maoni haya ya rasimu yepi yalikuwa maoni ya CCM? nahitaji kujua hilo! Maana naona maoni karibia yote ni mwiba kwa CCM!

Ni huu ushabiki wa kisengerema ndio uliotaka kuharibu zoezi hapo awali, tutenganishe kabisa siasa na uandishi wa katiba maana tutaharibu zoezi hili. Kwa taarifa yako muongozo wa kutoa maoni ya katiba kwa wana ccm ni kama umepigwa photocopy tu kwenye hii rasimu.
 

Mimi kwangu kilichonivutia ni pale kwenye Madaraka ya Raisi yanabaki kama yalivyo hapo tu, Mimi binafsi napinga kuvunja vunja Madaraka ya Raisi, sitaki kuishi kwenye Nchi ambayo hakuna mtu mwenye NENO la Mwisho! Hivyo nakubaliana na hii Rasimu!
 
Daah kuna ulaji tena wa kuandaa katiba Tanganyika? Itabidi tufanye mipango nasisi tuwemo humo kama kina Humphrey Harakaharaka.

Mkuu hiyo inakuja!ZNZ wenyewe tayari wanayo hadi katiba kamili!Nahisi tutapiga kura ya maoni kama jina letu la Tanganyika lirudi au tuitwe tu Tanzania Bara!

Ulaji huo lkn nahisi itakuwa ngumu kidogo kupenyezewa ulaji kuwa mjumbe wa Tume hiyo la sivyo uwe na sifa za u-jaji!
 
kwa kuwa hii ni RASIMU YA MAPENDEKEZO sio kwamba ndio imeshakuwa KATIBA RASMI ahhh tutaijadili huko kwenye mabaraza ya katiba kwa nguvu zote hata mimi naweweseka na serikali 3, ni MZIGO kwa Taifa na athari zake ni kubwa kwa Taifa zima.
-pia athari zake MGOMBEA BINAFSI KWA NAFASI YA U-RAIS ni kubwa pia so haya ni mambo mawili nitajadili kwa kina katiba baraza la katiba wilaya. kwa kuwa ni mjumbe sina shaka watanielewa wajumbe wenzangu tutaelewana na kushauri wengine kuliona hili kwa jicho la mbali zaidi...................Mungu ibariki Tanzania......!!!
 

Daa hivi ni lazima kuwaza haya majina mawili tu? Mimi ningependa tutunge jina jipya lisilo na chembe za ukoloni kama hili la Tanganyika.
 
hii katiba mpya utafikiri imeandikwa na chadema. katiba ina mambo yale chadema iliyo yapendekeza sema baadhi yamebadilishwa kimuundo tu. mia
 
Daa hivi ni lazima kuwaza haya majina mawili tu? Mimi ningependa tutunge jina jipya lisilo na chembe za ukoloni kama hili la Tanganyika.

Rasimu ya Katiba Mpya imesisitiza kuhusu kuutambua UTU WETU na HESHIMA;watasema tukileta jina jipya kabisa basi HATUUTAMBUI UTU wetu na TULIPOTOKA ahahahahaha
 
Rasimu ya Katiba Mpya imesisitiza kuhusu kuutambua UTU WETU na HESHIMA;watasema tukileta jina jipya kabisa basi HATUUTAMBUI UTU wetu na TULIPOTOKA ahahahahaha

Nitakubaliana nao kama watanishawishi kuwa hakuna mkono wa mkoloni kwenye jina la Tanganyika, la sivyo jina hili linatudhalilisha sisi na utu wetu.
 
Mwenye hyo draft atupe tuipitie maana warioba kataja machache tu asije ikawa kataja yale yaliyopendwa kusikika na majority ila yale ambayo wananch hawayaki na kuyapinga kwenye maoni hayajasomwa lkn yapo kwenye rasimu.
 
sikubaliani na hoja kwamba ukanda utaleta ukabila na udini,huu ni ufinyu wa kuangalia, kjiona kwamba sisi ni wakanda fulani hilo na kubaliana nalo kama ilivyo tunapojiona kwamba sisi ni wa mkoa fulani au wilwya fulani,lakini ukabila utakuwa hauna nafasi kwa sababu ukanda unachanganya makabila mengi na dini nyingi, kama ni ukabila ungeletwa na mikoa au wilaya maana hii ndio inaweza kukuta wilaya ina kabila moja au mkoa una kabila chache sana, sasa kama hatukuweza kuwa na ukabila kwenye umikoa wenye kabila chache tutawezaje kuwa na ukabila kwenye ukanda wenye kukusanya makabila mengi?. suala la ukanda ndio suluisho la ufisadi
 


Kwa nini Mawaziri 15 wakati mambo ya Mungano ni 7 tu?
na hata ukiangalia hapo mambo ya muungano yatakayo itaji Mawaziri haya Zidi 5, kwavyovyte ilitakiwa Mawaziri wasizidi 10 na sio 15.
 
serikari ya majimbo wanaikwepa tu kwa kisingizio na hoja nyepesi lakini Utawala wa Majimbo ni wa Gharama nafuu zaidi ya serikari tatu endapo watazingatia Majimbo mawili

Magamba wamebanwa kila mahali. Hii tume inakua kama kiini macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…