Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu kada wa CHADEMA amepanda cheo kuwa msemaji na accountant wa CHADEMA!
Katika kile kinachoonekana kutapatapa kwa CCM Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nauye amekishushia tuhuma Chama kikuu cha upinzani nchini Chadema.
Akizungumza katika kongamano la katiba jana Nape anasema amepata taarifa za uhakika kwamba kiongozi mmoja wa Chadema alienda nje ya nchi mwezi uliopita na kupewa mabilioni ya fedha kwa lengo la kuja kuvuruga mchakato wa Katiba mpya unaoendelea.
Nape amesema kiongozi huyo wa Chadema alisafiri tu mara pale Tume ya Katiba ilipotoa Rasimu yake na aliporudi ndipo chokochoko za kuvuruga mabaraza ya katiba zilipoanza.
Nape ametamba kwamba njama zote hizo zitazimwa na chama chake.
Source:Nipashe Jumapili.
Hana ujasiri wa kusimama kwenye debate.Saizi yake facebook na jukwaa la TOT kunengua na Gitaa kunogesha mipasho au mziki wa mwambao.Hapa tunamuonea tu kwa tunaomfahamu.