Mimi siwaelewi chadema kabisa na watanzania wanaoshabikia hili
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 CHADEMA walitangaza kutokubali matokeo na kuamua kususia kila kitu kilichotokana na uchaguzi huo kwa kufanya yafuatayo.
1. walitangaza kutomtambua raisi
2. Walimzuia mbunge wa nkasi kwenda bungeni
3. walitangza kususia nafasi za ubunge wa viti maalumu
4. Walitangaza kususia ruzuku.
Baada ya kufanya haya
Chama kiligawanyika katika makundi kulingana na maslahi
1. Mbunge wa nkasi alikataa kutii na kuwaeleza kuwa yeye alichaguliwa na wananchi wa nkasi hivyo alikwenda bungeni kuwawakilisha wananchi wa nkasi.
2. Wanawake waliotegemea nafasi za viti maalumu walikataa hoja za kususa kwa hoja kwamba msiamo wa chama chaguzi zote umekuwa wa kukataa matokeo, kipindi hicho viongozi walipokuwa wakipata nafasi za ubunge hawakuleta hoja za kususia fursa hizo ila baada ya kukosa wanataka kila mtu asuse.
Wanawake waliona kama kuna doble standard katika maamuzi na hivyo kuamua kutosusia nafasi za ubunge wa viti maalumu. Hapa Chadema walianzisha mchakato wa kuwatimua bungeni kwa kwanza kudai hawajawateua, hoja hii ilipogonga ukuta wakawafukuza chama kwa kutegemea watakuwa wamekosa sifa za kuwa wabunge.
3. Viongozi wa juu wa chama, Mwenyekiti pamoja na Makamu mwenyekiti wamekutana na raisi mara kadhaa ikiwemo kwenda ikulu. hii inaonyesha viongozi wa juu nao wametupilia mbali msimamo wa kutotambua matokeo ya uchaguzi.
4. Chama kumwandikia spika wa bunge barua ni sawa na kutambua pia matokeo ya uchaguzi kwa maana kama hutambui matokeo ya uchaguzi na kitu chochote kilichotak kwenye matokeo ya uchaguzi huwezi kumwandikia "official letter" mtu anayeshika wadhifa uliotokana na matokeo ya kura.
Lakini yote bin yote ni hii hatua ya CHADEMA kutafuta serikali / Bunge kuwaunga mkono wao waliosema hatutambui matokeo ya uchaguzi na fursa zitokanazo na matokeo ya uchaguzi kwa kuwafukuza wabunge 19 ambao wao walikaa upande wa serikali na bunge kwa kutambua kila kitu na kuchukua fursa.
Je, inawezekana serikali ikawaunga mkono kwenye kivuli cha katiba inavunjwa?
Je, katiba inawapa ruhusa wanachadema kugoma na inawanyima ruhusa baadhi ya wanachadema kukataa kugoma?
Je, mwenyekiti anavyokwenda ikulu kuzungumza na mama wakati chama kilishatoa msimamo wa kutotambua serikali, je naye anatakiwa kuchukuliwa taratibu za kinidhamu na chama?