CHADEMA wanapaswa kwenda Butiama kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere

CHADEMA wanapaswa kwenda Butiama kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Kwa vile CHADEMA wapo Mara, ingefaa kama wangekwenda kulizuru kaburi la Mwalimu. Kwa sababu inafaa kama watu wanafanya shughuli za kisiasa Mara wapite kumsabahi Mwalimu. Inafaa watu wanaotaka kuongea na Watanzania,waende kwanza kumsabahi Mwalimu. Inafaa watu wanaotaka kuongea na Foreigners kuhusu masuala ya kisiasa ya Tanzania, wamsaluti kwanza Mwalimu Nyerere.

Kumbuka Mwalimu Nyerere alisema,"Wazo la kuanzisha Vyama Vingi ni wazo zuri. Nitafurahi kama CCM watalipa serious consideration". Akasema pia Mwalimu,"Uingereza vyama vya Upinzani vilipoanzishwa vilileta mgogoro. Halafu Waingereza wakaamua kuruhusu Upinzani. Wakasema tutaiita His Majesty'Opposition Party.

Kwa maana kwamba kile Chama kinapinga mambo yanayofanywa na Chama Tawala,kama vile dhuluma,au mfumuko wa bei,ambayo hata mfalme akitazama kutoka Buckinham Palace,yeye pia anapinga.

Sasa hivi Madaraka Nyerere hayupo Butiama,amekwenda Cuba jana, lakini wapo wengine wa kuwapokea.
 
Nyerere ndio source ya matatizo mengi yaliyopo Sasa, swala la katiba ni yeye ndio angewwka msingi wa katiba bora tusingekuwa hapa.

Kwanza ni lazima ufahamu si kila mtu ni muabudu mizimu, kaburi la Nyerere lina nini mpaka mtu uende hapo?
 
Waende Chato kwenye kaburi la Magufuli wakatubu dhambi ya kushangilia kifo chake.
 
Braza Andrew mzee huoni tunamsumbua na upo hapa kutupa ruhusa tukamsumbue zaidi.
 
Back
Top Bottom