tang'ana
JF-Expert Member
- Apr 3, 2015
- 11,931
- 15,849
Wafuasi wa CHADEMA wanaofika katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wao Freeman Mbowe na wenzake watatu wamebuni utaratibu wa kuandaa na kupata mlo wakiwa mahakamani hapo.
Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi ikiwemo kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi na kesi yao imeahirishwa.
Utaratibu waliobuni wafuasi hao ni kuchangishana fedha kwa ajili ya kununua mihogo, viazi na maji ya kunywa ambapo hukabidhiwa kwa mwanachama mmoja aliyejitolea kupika nyumbani kwake na asubuhi huenda navyo mahakamani hapo. Wafuasi hao hupata mlo huo wakati wa mapumziko ambapo hukaa pamoja na kula nje ya mahakama hiyo.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Novemba 16,2021, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha Kanda ya Pwani Patrik Assenga amesema kesi inayomkabili Mbowe ni ya ugaidi hivyo watu wengi hasa wanachama kutoka maeneo mbalimbali wanapenda kwenda kufuatilia.
Wanaoguswa wanachangia chochote walichonacho angalau makamanda wapate kutafuna viazi na mihogo ili mchana upite wasipate tabu sana, watu wengi wameguswa na wanaendelea kuchangia," amesema Assenga.
"Tunatoa wito hatutaki vijana wetu waendelee kupata tabu, tunataka waendelee kukaa kwa raha…. usiseme wanakula viazi mpaka lini bali tambua kuwa hatua itakayofuata watu wetu watakula biriani," amesema.
Mwanachama aliyejitolea kupika mihogo hiyo Hadija Mwampalile amesema amejitolea kupika kutokana na namna anavyoipenda Chadema kutoka akiwa mdogo wakati huo Mbowe anagombea urais.
" Jukumu la kupika mihogo nililipata baada ya kiongozi wangu kutafuta mtu wa kupika basi nikajitolea naamka saa kumi natafuta viazi au mihogo namenya naikaanga tena kwa kutumia gesi kwa saa mawili na inapofika saa moja asubuhi ninakuwa nimeshafika mahakamani," amesema Mwampalile.
Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa baada ya Jaji Joachim Tiganga kushindwa kukamilisha kuandika uamuzi kutokana na wingi wa hoja zilizotolewa na mawakili wa pande zote mbili.
Source: Mwananchi online la 16/11/2021.