CHADEMA wanazo sababu za kumpongeza Rais Samia kwa hotuba yake badala ya kulalama!

CHADEMA wanazo sababu za kumpongeza Rais Samia kwa hotuba yake badala ya kulalama!

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwamba kumbe nini kilitumainiwa?

Kwamba Chadema kama ilivyo kwa wananchi wengine wamekuwa wanachukizwa mno na tekaji tekaji hizi?

Kwamba Chadema kama ilivyo Kwa wananchi wengine wanaona ni muhimu uchunguzi huru na wa haraka kufanyika sasa?

Kwamba Chadema kama ilivyo kwa wananchi wengine hawakubaliani kuwa kifo cha Mzee Kibao ni kifo tu?

Kwamba polisi au Samia hawataki kusikia miito ya uchunguzi huru?

Kwamba polisi au Samia wanaona kifo cha Mzee Kibao ni kifo tu kama vingine?

Kwamba kumekuwa na tashwishi ya kuwa vyombo vya dola vinahusika?

Kwamba kumbe basi, kwa hotuba yake kungetegemewa kipi kigeni?

Katu huu haukuwa muda wa kulalama.

Huu ulikuwa muda wa kububujikwa machozi, kumpa pongezi na kumtaarifu kwa hotuba yake ya jana, Sep 23 ni muhimu zaidi, kuliko hata awali Ili kuwafikishia ujumbe wote wasioelewa.

"Uchunguzi huru ni kwa masilahi pia ya watuhumiwa wote."
 
Back
Top Bottom