GE2025 CHADEMA wataka anayedhaniwa kuwa Polisi atolewe nje ya Mahakama

GE2025 CHADEMA wataka anayedhaniwa kuwa Polisi atolewe nje ya Mahakama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
K
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakiomba kutolewa nje mtu mmoja aliyedhaniwa ni askari ambaye ameenda kukaa katika benchi la wafuasi hao

Leo Septemba 8, 2025 Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anapandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (preliminary hearing) wa kesi ya uhaini inayomkabili




Chanzo: Mwananchi_official
huu ndio upumbavu wa chadema sasa polisi hana haki ya kuhudhuria mahakamani

USSR
 
Wewe unaamini polisi wote 45k ni maadui wa chadema??

Kuna watu ni cdm kamati kuu wana ndugu polisi,kuna watu ni maafisa wakubwa polisi wana ndugu ambao ni cdm kufa kupona.

Kuna maisha mengine nje ya hizi siasa.

Afande hivi bado upo kwenye cheo chako Cha ukoplo?
 
Hivi polisi akiwa off, hana haki ya kwenda kusikiliza kesi mahakamani kama raia wengine? Au mtu akiwa polisi anapoteza haki nyingine zote?

Chadema msijekuwa mnafukuza malaika mkidhani ni shetani!
Kwa kweli aliwalaumu CHADEMA binafsi siwalaumu. Acha wajihami serekali ya CCM na taasisi zake inavyo wa treat si kwa haki kabisa. Wanaotekwa na kuuliwa, kubambikiwa kesi, hujuma kama zote?
 
Hivi polisi akiwa off, hana haki ya kwenda kusikiliza kesi mahakamani kama raia wengine? Au mtu akiwa polisi anapoteza haki nyingine zote?

Chadema msijekuwa mnafukuza malaika mkidhani ni shetani!
Mmmmmmm
 
Wewe unaamini polisi wote 45k ni maadui wa chadema??

Kuna watu ni cdm kamati kuu wana ndugu polisi,kuna watu ni maafisa wakubwa polisi wana ndugu ambao ni cdm kufa kupona.

Kuna maisha mengine nje ya hizi siasa.
Mapitio wanayopitia hawa CHADEMA na serekali ya CCM ni lethal kunawatu wameuawa kwasababu tu wapo CHADEMA, kuna wajane na yatima wakutosha waliopatikana kisa tu wenza/ wazazi wao wako CHADEMA!
 
Kwamba chadema ndio wamejua leo kwamba wanafuatiliwa😂😂,ujute hapo wako 5,wamemhisi mmoja tu.
Halafu wamenifurahisha eti wanasema onyesha alama yao kama ujafanya ni mamluki, ndio jamaa amekamatiwa hapo ajanyosha 😄
 
Hivi polisi akiwa off, hana haki ya kwenda kusikiliza kesi mahakamani kama raia wengine? Au mtu akiwa polisi anapoteza haki nyingine zote?

Chadema msijekuwa mnafukuza malaika mkidhani ni shetani!
Wao wanapoktaza wengine huwa hawajui hiyo haki?
 
Kwahiyo kama ni kweli ni polisi, polisi haruhusiwi kuwa mfuasi wa chadema wala kusikiliza kesi,au point husika hapa ni ipi??
Mkuu sahivi mtu yuko radhi akutane na jambazi sio polisi. Watu wanaogopa kutekwa, maana unaweza ukatoka humo ndani ukafuatwa hadi makazi yao.

Ndio tulipofikia, juzi nilikua kwenye basi polisi wakasimamisha ile wanaingia ndani kila mtu akawa na wasiwasi maana walihisi wanaweza tekwa kama Ali kibao.

Imagine we are not safe around police
 
kwani ili awe mfuasi anatakiwa asiwe polisi??kwani chadema wanajua kazi za wafuasi wao wote???
Wenye chama chao wanajuana nani ni nani, kwa akili ya kawaida umeona wapi Askari anavaa nguo yenye nembo ya chadema anatembea mtaani au yupo kwenye tukio maalumu kama hili? Basi huyo atakuwa hapendi kazi yake.
 
Mkuu sahivi mtu yuko radhi akutane na jambazi sio polisi. Watu wanaogopa kutekwa, maana unaweza ukatoka humo ndani ukafuatwa hadi makazi yao.
Hujawahi ibiwa hata simu mkuu ndio maana unaandika haya.
kuhusu kutekwa unazuiaje mbinu za watekaji kwa kupiga makelele kwamba umeshtuka uko na polisi mahakamani😁😁.
Ndio tulipofikia, juzi nilikua kwenye basi polisi wakasimamisha ile wanaingia ndani kila mtu akawa na wasiwasi maana walihisi wanaweza tekwa kama Ali kibao.
Kuhisi hauko safe ni akili za kawaida kabisa,usikae kizembe hata siku moja.
uwe karibu na polisi,jambazi au hata hao chadema wenzio kaa kimkakati.
Imagine we are not safe around police
 
Wenye chama chao wanajuana nani ni nani, kwa akili ya kawaida umeona wapi Askari anavaa nguo yenye nembo ya chadema anatembea mtaani au yupo kwenye tukio maalumu kama hili? Basi huyo atakuwa hapendi kazi yake.
Wacha nikwambie,polisi wapo,nguo zote wanavaa hata za ccm,tofauti yao na wewe hawavai ili wapendeze.
 
Kwahiyo kama ni kweli ni polisi, polisi haruhusiwi kuwa mfuasi wa chadema wala kusikiliza kesi,au point husika hapa ni ipi??
{...pointi husika...", ni hiyo ambayo hata wewe hukutaka kuitaja.
Sasa bado utasema huelewi. Sitakushangaa!
 
Hivi polisi akiwa off, hana haki ya kwenda kusikiliza kesi mahakamani kama raia wengine? Au mtu akiwa polisi anapoteza haki nyingine zote?

Chadema msijekuwa mnafukuza malaika mkidhani ni shetani!
Eti unasemaje, mkuu 'sex''? Huyo polisi anaweza kuwa off-kimavazi huku akiwa kazini?

Nami ngoja nikoleze hoja yako kwa kuwasihi CHADEMA wawakaribishe na wenzao ccm humo mahakamani kusikiliza kesi.
Kimsingi hakuna la kushangaza sana ikitokea hivyo; na nadhani kwa maoni yako hapo mahala patakuwepo na undugu mkubwa sana baina yao.
Sasa kwa polisi, katika mazingira ya sasa wanayopitia CHADEMA; nadhani unapendekeza hawa watu wageuke kuwa malaika.
 
Back
Top Bottom