GE2025 CHADEMA wataka anayedhaniwa kuwa Polisi atolewe nje ya Mahakama

GE2025 CHADEMA wataka anayedhaniwa kuwa Polisi atolewe nje ya Mahakama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Eti unasemaje, mkuu 'sex''? Huyo polisi anaweza kuwa off-kimavazi huku akiwa kazini?

Nami ngoja nikoleze hoja yako kwa kuwasihi CHADEMA wawakaribishe na wenzao ccm humo mahakamani kusikiliza kesi.
Kimsingi hakuna la kushangaza sana ikitokea hivyo; na nadhani kwa maoni yako hapo mahala patakuwepo na undugu mkubwa sana baina yao.
Sasa kwa polisi, katika mazingira ya sasa wanayopitia CHADEMA; nadhani unapendekeza hawa watu wageuke kuwa malaika.
Mkuu nilikuwa natoa angalizo tu kwamba yawezekana ni askari mwenye mapenzi mema na Lisu pamoja na mabadiliko
 
Polisi anataka akitoka hapo apeleke taarifa za makamanda watekwe! Safi, vizuri wamemsanua.. 😊
 
Mkuu nilikuwa natoa angalizo tu kwamba yawezekana ni askari mwenye mapenzi mema na Lisu pamoja na mabadiliko
Inawezekana; na sina shaka yoyote wapo polisi wengi sana walio na hali hiyo. Lakini, kutokana na uhalisia ulivyo sasa; mtu wa namna hiyo kujichanganya tu kwenye kundi linaloteswa, bila hata ya baadhi ya hao wanaoteswa kujuwa anasimamia wapi; hapo ni kutaka tu kuwatupia lawama CHADEMA.
Kumbuka, ni hawa hawa walikusanywa hapo mahakamani na polisi na kupelekwa porini kwenda kupondwa miguu!

Hali ni mbaya mkuu; katika uhusiano wa polisi (viongozi) na wafuasi wa chama.
 
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakiomba kutolewa nje mtu mmoja aliyedhaniwa ni askari ambaye ameenda kukaa katika benchi la wafuasi hao

Leo Septemba 8, 2025 Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anapandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (preliminary hearing) wa kesi ya uhaini inayomkabili




Chanzo: Mwananchi_official
Ni ujinga wao waangalie na kusikiliza kama Kesi imeenda sawa sawa haya mambo ya kujifanya mnachukia kila mtu kwa kigezo cha kuwaona ni wa Serikali ni kujipunguzia ushirikiano wa kitaasisi
 
Hujawahi ibiwa hata simu mkuu ndio maana unaandika haya.
Nimeshaibiwa ila hao polisi hawakusaidia chochote na walikula laki 2.5 zangu na bado wakadai nyingine na huku kazi hawakufanikisha.
kuhusu kutekwa unazuiaje mbinu za watekaji kwa kupiga makelele kwamba umeshtuka uko na polisi mahakamani😁😁
Unaanza kufuatiliwa baadae unatekwa unalawitiwa alafu unatupwa msituni. Nani yupo tayari kupakwa wese mzee?
Kuhisi hauko safe ni akili za kawaida kabisa,usikae kizembe hata siku moja.
uwe karibu na polisi,jambazi au hata hao chadema wenzio kaa kimkakati.
Hapana, ilipaswa kufeel safe around the police not otherwise
 
Ni ujinga wao waangalie na kusikiliza kama Kesi imeenda sawa sawa haya mambo ya kujifanya mnachukia kila mtu kwa kigezo cha kuwaona ni wa Serikali ni kujipunguzia ushirikiano wa kitaasisi
Ngoja siku uingie 18 za polisi ndio utaelewa kwanini watu wanakosa amani wakiwa karibu na polisi.
 
Nimeshaibiwa ila hao polisi hawakusaidia chochote na walikula laki 2.5 zangu na bado wakadai nyingine na huku kazi hawakufanikisha.
Kwanini uliwapa hela kufanya kazi ambayo wanalipwa kwayo??unaona namna ambavyo unakuwa mshirika wa mabaya amabyo polisi wanalalamikiwa nayo??unatoa hela ili kuhalalisha nini??
Unaanza kufuatiliwa baadae unatekwa unalawitiwa alafu unatupwa msituni.
mkuu,kama watu wana nia ya kukuteka wakupake wese,niamini mimi wala huwezi shtuka,lah sivyo unajua kibaya kulichokifanya.
Nani yupo tayari kupakwa wese mzee?
Hapana, ilipaswa kufeel safe around the police not otherwise
Swala la kufeel safe polisi ni la kiasili,haliwezi kuondolewa kwa style hiyo,kama huamini ushikwe kwa tuhuma za wizi halafu uone polisi wanatokeza,utashukuru badala ya kulia.
 
Huyo "polisi" mwenyewe mbona kama dishi limeyumba...
 
Kwahiyo kama ni kweli ni polisi, polisi haruhusiwi kuwa mfuasi wa chadema wala kusikiliza kesi,au point husika hapa ni ipi??
Unaandika ukiwa wapi? Polisi wa CCM anawezaje kuwa CHADEMA!? Kada zote zinaweza kuwa na wanachadema ila siyo polisi
 
Hivi polisi akiwa off, hana haki ya kwenda kusikiliza kesi mahakamani kama raia wengine? Au mtu akiwa polisi anapoteza haki nyingine zote?

Chadema msijekuwa mnafukuza malaika mkidhani ni shetani!
Shetani hafananishwi na malaika
 
Back
Top Bottom