Chadema wataka Television ya taifa (TBC) iwe inarusha ibada mubashara siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ili kuepusha misongamano Ibadani

Chadema wataka Television ya taifa (TBC) iwe inarusha ibada mubashara siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ili kuepusha misongamano Ibadani

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Chadema imesema ni wakati sasa wa Runinga ya taifa kuwatumikia Wananchi kwa kuwapa fursa ya kufuatilia Ibada mubashara wakiwa majumbani mwao.

Hayo yamesemwa na mbunge wa Geita na Naibu waziri kivuli mh Upendo Peneza alipoongea na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Upendo amesema Waislamu wataitumia siku ya Ijumaa, Wasabato Jumamosi na Wakristo wengine Jumapili na kwamba ni wajibu wa viongozi wa TBC kukutana na viongozi wa dini ili kuweka utaratibu kwani madhehebu kwa kila dini yapo zaidi ya moja.

Upendo amesisitiza kuwa hatua hii itawafanya waumini wengi kushiriki Ibada pasipo kuhudhuria kwenye nyumba za Ibada na hivyo kuondoa msongamano.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Kama masuala ya Afya wataalamu husika ndio hupaswa kuyatolea maaelezo basi na masuala ya imani za watu pia utaratibu huo wa kuachia wataalamu husika nako usingatiwe.
 
johnthebaptist,

Unadhani hawakulijua hilo mapema tatizo lao wanawaza SADAKA (Na bahati mbaya saana Serikali nayo imeingia mtegoni katika hili kwa sababu za kisiasa).

Ni waumini wachache wapo tayari kutuma MPESA kama sadaka arafu kuna dini nyingine kama kanisa katoliki hawajazoea utaratibu huu wa MPESA.

Akili za Kawaida zinanisukuma kujiuliza kwanini viongozi wa dini wasingezuia ibada za Dar es salaam, Arusha na Zanzibar kwa kuanzia na kuruhusu Mikoa mingine tu ambayo haijadhurika waendelee na ibada kama kawaida?

Jibu ni kwamba Sadaka ya Dar es salaam peke yake ni zaidi ya mara 200 ukichanganya mikoa iliyobaki yoote (Ukitoa Arusha na Mwanza)
 
Kama masuala ya Afya wataalamu husika ndio hupaswa kuyatolea maaelezo basi na masuala ya imani za watu pia utaratibu huo wa kuachia wataalamu husika nako usingatiwe.
Soma historia ya Kanisa uone jinsi mambo mengi tena ya muhimu sana, yalivyoanzishwa na waumini wa kawaida (walei).

Na hili la kusali siku 3, limetolewa na kiongozi wa kanisa? Usinambie Magufuli ni Askofu!!
 
Sio TBC tu; kutokana na janga lililopo ilitakiwa TV na radio stations zijiongeze. Wangekutana wakurugenzi na kukubaliana namna ya vituo vyao kuchangia katika janga hili mojawapo eneo la imani.

Wakijua watanzania ni watu wanaopenda sana kuabudu hususan wale wenye dini zao, walitakiwa wawe wameshakamata fursa siku nyingi na wangekuwa wametoa mchango wao mkubwa tu katika kupambana na janga hili.
 
johnthebaptist,

Bhagosha, kumbe TBC ni televisheni ya taifa nilijua ni ya CCM. TBC haifanani kabisa na televisheni ya taifa kwa namna wanavyorusha matangazo yao
 
Sio TBC tu; kutokana na janga lililopo ilitakiwa TV na radio stations zijiongeze. Wangekutana wakurugenzi na kukubaliana namna ya vituo vyao kuchangia katika janga hili mojawapo eneo la imani. Wakijua watanzania ni watu wanaopenda sana kuabudu hususan wale wenye dini zao, walitakiwa wawe wameshakamata fursa siku nyingi na wamengukuwa wametoa mchango wao mkubwa tu katika kupambana na janga hili.
Nimekuelewa!
 
Upendo amesema Waislamu wataitumia siku ya Ijumaa, Wasabato Jumamosi na Wakristo wengine Jumapili na kwamba ni wajibu wa viongozi wa TBC kukutana na viongozi wa dini ili kuweka utaratibu kwani madhehebu kwa kila dini yapo zaidi ya moja.
Angetoa idadi ya juu ya madhehebu ya dini ndio labda ningemwelewa zaidi na kuona kama wazo lake lina tija. Pia anafahamu kuwa kama sikosei TV viewers nchini yaweza kuwa asilimia 25 au chini ya population ya Watanzania?

Badala ya TBC, dini na madhehebu yafungue TV na radio stations (kwa redio mengine tayari) zao, na kutumia Internet ku-stream ibada zao kwenye instagram, facebook, youtube, n.k.
 
Back
Top Bottom