Nashauri kuwe na Kipindi Maalum cha Neno la Mungu kila siku kwa njia ya Televisheni (TBC1), kwa muda wote wa kipindi hiki cha Corona
- Kiwe kinahudumiwa na watumishi wa Mungu wa dini zote kubwa hapa nchini, Waislamu na Wakristo
- Kama Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa hataniadhibu kwa kumpangia majukumu, napendekeza awe ndiyo coordinator wa kipindi hiki, akiziunganisha dini (na Madhehebu yake), na Serikali, yaani TBC1. Uzoefu wa pekee alioupata wakati alipowakutanisha viongozi wa dini mwaka jana ndiyo unaonifanya nitoe pendekezo hili
Watumishi wengine ninaopendekeza Mh. Mkuu wa Mkoa ashirikiane nao kwenye kamati yake kwa kuanzia ni
1. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam (mwakilishi BAKWATA)
2. Mch. Anthony Lusekelo (mwakilishi FPCT)
3. Padre Dr. Kamugisha (mwakilishi TEC, kama yupo hapa Dar es salaam, au Padre mwingine yeyote atakayetoka TEC)
Vipindi virekodiwe na watumishi wa Mungu/ wahusika wa kutoa neno halafu vitumwe kwa njia ya mtandao TBC1, kwa sababu ya Corona
TBC1 kama wataridhia, watoe ile saa 1 ya mwanzo ya kile kipindi kipya cha ARIDHIO, ndiyo kitumike kwa ajili ya NENO la Faraja kwa wa-Tanzania, mpaka pale Corona itakapokuwa imeteketea kabisa.
Nusu saa iwe ni kwa ajili ya neno kutoka maandiko matakatifu ya Quran, na nusu saa nyingine tena iwe ni kutoka kwenye maandiko matakatifu Biblia
Kwa upande wa Wakristo, watumishi wafuatao wahamasishwe kuhakikisha kuwa wamerekodi vipindi vyoa na kuvituma TBC1
Baba Askofu Pengo, na maaskofu wengine wa majimbo yote Katoliki Tanzania nzima
Maparoko wote Tanzania
Wachungaji wote, wakiwemo wale ninaowafahamu mimi kama
Mch Dr. G Rwakatare, Mwalimu Mwakasege, Mch. Allen Mbiso (KKKT Mbezi Beach), Mchungaji Kimaro (KKKT Kijitonyama), Mchungaji Mayala (TAG Tabata Kisukulu), Mch. Mosses Maghembe (TAG Ukonga), Mch. Paul Mlokozi (TAG Ubungo), Mch Dr. Alex Malasusa (DMP) na wengine wengi
Kipindi kiwe kinaruka kila siku saa 1 mpaka saa 2, muda mzuri ambao watu wengi wanakuwa wamesharudi nyumbani kutoka maofisini.
Theme ya kipindi isiwe maombi, bali neno lolote la faraja kwa ajili ya wa-Tanzania katika kipindi hiki cha COVID-19, mpaka itakapopita. Neno lenye kuchambuliwa kwa kina na watumishi wa Mungu waliobobea
Naomba kuwasilisha