Mkuu kuna mambo na nyakati ambazo hazihitaji hisia za chama, udini au ukabila, moja wapo ni maafa ya asili kama haya mafuriko ya Hanang.
Mosi, weka ushahidi hapa kuwa kweli wananchi wanachama wa Chadema waliopo maeneo hayo hawajaadhirika?
Pili, weka ushahidi bayana hapa kuwa kweli wananchi wanachama wa Chadema walio salimika hawaja saidia majirani zao waliodhurika kwa namna yoyote. Au wamewasaidia kwa ubaguzi wa itikadi ya kichama.
Tatu, weka ushahidi wazi hapa kuwa kweli wananchi viongozi wa Chadema wa mashina, vitongoji, vijiji/mitaa, kata, wilaya, mkoa na kanda mmoja mmoja au kwa Makundi yao hawaja dhurika? Au kweli hawaja shiriki kusaidia kutoa msaada kwa waadhirika? Au kweli hawajashirikiana na wananchi wengine kwenye zoezi zima la uokoaji hapo Hanang?
Nne, kwa uwazi ainisha hapa kuwa kwa mujibu wa sheria ni nani mwenye wajibu wa kushughulika na maafa kifedha na kitaalam? Au Kisheria ni nani aliyetengewa fedha ya kushughulika na masfa ya asili?Je, ni vyama vya siasa? Au serikali?
Tano, je watu kutoa maoni yao, kukumbusha waokoaji na kwa ujumla kushauri jinsi zoezi la uokoaji linavyoendelea huko Hanang kupitia hapa mitandaoni ni jambo baya?
Je hata wewe ulivyo toa maoni yako hapa mtandaoni unafikiri umefanya vibaya?