Naunga mkono hoja, kwenye majanga ya Kitaifa, lets stand united as one, kushikana mikono kusaidia na kusaidiana!.
P
Stand united...!?
What exactly do you mean? Do you mean we have to stand united kujiunga kwenye ujinga na upumbavu wa viongozi wa serikali hii..? Really?
NO WAY..!
Kwa akili yako wewe ndugu
Pascal Mayalla na huyu mleta mada
sinza pazuri katika hali ya janga hili lililowapata kweli mnadhani wananchi wa Katesh -Hanang na vijiji vilivyoathiriwa hawako united licha ya kuwa wana tofauti zao za itikadi za kisiasa na kiimani..?
Kama mnadhani hivyo, basi bila shaka nyie ni wanafiki na wapuuzi wa kupindukia...!
On the other hand, kumbukeni kuwa nchi hii ina special department inayohusika na majanga...
Lakini badala yake nini kinachoonekana huko Katesh Hanang?
Ni ujinga, upumbavu na ulimbukeni mtupu wa viongozi wetu. Ni kama ujinga na upumbavu ulivyofanyika kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenda Dubai na msururu wa watu 700+ wakifuja fedha tu bila sababu zozote za msingi...
Yaani viongozi wetu hawa wajinga, wamekwenda kule kwenye scene ya maafa na msururu mrefu wa magari ya kifahari (Land cruiser V8) huku wakiwa wamevalia suti na wengine sare za kijani za CCM badala kutumia fedha hizo zilizoendesha magari na gharama za safari zao kuwapa professional people wawahi kwenye tukio kuokoa maisha ya watu...!
Katika mazingira haya kweli mnataka watu wanyamaze tu wasuseme na kuulaani ujinga na upumbavu huu nanyi mnakuja na hoja za "let's stand united..!!?. Yaani tuwe united kushabikia ujinga na upumbavu wa viongozi hawa??
NO WAY..!!
Watu walitarajia kuona helcopter zenye mahema, maturubai, vyakula, maji nk nk zikishambulia anga kuelekea kwenye tukio..
Watu tulitarajia tuone msururu wa magari special planes zikiwa na watu na vifaa vya wokozi kwa wingi vikifika haraka na kwa wakati kwenye tukio...
Usishangae hata hilo greda la kijiko serikali ime hijack kwenye makampuni binafsi ya ujenzi wa barabara na kulitaka lifanye kazi hiyo..
Sikiliza ndugu
Pascal Mayalla...
Hii weakness ya idara ya kukabiliana na majanga ya asili na ya ghafla ilijionesha na kuiacha serikali uchi wakati wa tukio la ndege ya Precision Air ilipoanguka Ziwa Victoria mwaka juzi..
Cha kushangaza, hali ileile tunaiona imejitokeza Tena kwenye janga hili huko Katesh - Hanang...
Serikali ifanywe nini ndipo ijifunze?
Au tunataka mpaka siku moja Rais Samia Suluhu Hassan ajikute ameanguka na ndege yake Bahari ya Hindi ili wavuvi wajaribu kumuokoa ndo tushituke na kujifunza??
Acheni hizo..