Katika maneno yaliyoandikwa chini ya hiyo picha kuna sentensi imeandikwa "Niwashukuru viongozi na wananchi ikiwemo na wagombea wenzangu wote kwa kuahidi kushirikiana nami".Mpaka sasa haieleweki nani mgombea ubunge halisi kupitia CHADEMA jimbo la Kilombero. Wakati kamati kuu ikimteua Modestus aliyeongoza kura za maoni kuwa mgombea uongozi wa kanda na wilaya umemkabidhi barua za kugombea ubunge Bilionea Nabii Daniel Shillah aliyeshika nafasi ya pili.
Tazama hapa nabii Shillah akipewa fomu
Kumbe wameshakubaliana na kuahidi kushirikiana, sasa wewe huo mvurugano umeutoa wapi? Hapo hakuna mvurugano ispokuwa kama utaleta kauli nyingine ya chama ama mtia nia mwingine inayosema tofauti na hiyo hapo juu.