CHADEMA Wazikana Kauli za Baraza la Wazee kwa kusema siyo Msimamo wa chama

CHADEMA Wazikana Kauli za Baraza la Wazee kwa kusema siyo Msimamo wa chama

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

CHADEMA kwa sasa ni kama wanajenga mnara wa Babeli.chama ni kama hakina uongozi wala hakifanyi vikao wala kuwa na mipango na mikakati ya pamoja . Ndio maana kila mtu hujitokeza hadharani kwa kukurupuka na mihemuko na kujiropokea chochote kile kinachomjia Mdomoni mwake bila utaratibu.

Ndio maana nyote ni mashahidi mliona Lissu akitoka hadharani na kujitolea zake maneno yaliyomjia Mdomoni mwake bila kufuata na kutumia vikao vya chama. CHADEMA ni kama wote ni makambale au mabeberu yaani kila mtu anajiona ana mamlaka zaidi ya vikao halali vyenye mamlaka ya kikanuni ,kisheria na kikatiba.

Ndani ya CHADEMA kila kitu ni ukurupukaji,Mihemko na utoto.kila mtu anataka kuongea ili apate sifa .ndio maana utaona kila mtu anajiandikia kwenye ukurasa wake mtandaoni na kuvalisha koti la chama .ndio maana chama hakina mwelekeo wala Dira . Chama kina kwenda tu kama kipofu gizani.Hakuna heshima wala kuheshimiana.hakuna heshima ya vikao wala kuheshimu vikao.ndio maana watu wanajikurupukia tu .

Hapa ndio muelewe kuwa ni CCM pekee yenye uwezo wa kuliongoza Taifa hili na likaendelea kutamalaki kwa amani,utulivu na mshikamano miongoni Mwa watanzania.watu kama CHADEMA wao tu hawawezi kujiongoza.sasa ni vipi wataongoza Taifa hili lenye watu zaidi ya Million 61.7?tusije tukarogwa kuwapa kura za ushindi hawa watu.hawa wanapaswa kuongozwa tu kwa kila kitu na kwa kila jambo

Screenshot_20241002-115731_1.jpg

======
Video yenye ujumbe wenye viashiria vya Kidini


 

Attachments

  • Screenshot_20241002-115731_1.jpg
    Screenshot_20241002-115731_1.jpg
    142.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom