Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Wanaukumbi.
CHADEMA hakina Sera ya chama madhubuti, kila mtu ni msemaji. Vijana wa CHADEMA kumtukana kila mtu anaejaribu kutoa maoni tofauti na chama chao, bila kujua mpiga kura huwa anabadilika kulingana na Sera za wakati uliopo.
CHADEMA wameshindwa kuendesha chama kama taasisi ya umma, kwa sasa chama kinaendeshwa kwa remote ya wanaharakati wa "Mchongo" na mihemko ya mitandaoni. Chama kinadaka kila tukio na kuligeuza ajenda ya kisiasa.
CHADEMA kiukweli kinahitaji mabadiliko makubwa sana (Massive Reform) inahitajika kubomoa mfumo na uongozi mzima uliopo sasa kisha kujenga chama upya. Wako vijana wana mioyo thabiti ya kupigania Haki, demokrasia na maendeleo ya watanzania. Vijana wanaojielewa na wenye elimu kuliko hawa wahuni wa sasa.
CHADEMA kitoke kuendeshwa kama genge la wanaharakati "Mchongo" (hardcore activists) na kuendeshwa kama chama cha siasa kinachojikita katika sera za kubadilisha maisha ya watanzania, kupigania demokrasia, haki, umoja, upendo na mshikamano. Siasa sio harakati.