Uchaguzi 2020 CHADEMA yaahidi kumtunza Dkt. Magufuli kama Rais Mstaafu

Uchaguzi 2020 CHADEMA yaahidi kumtunza Dkt. Magufuli kama Rais Mstaafu

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
17 September 2020

CHADEMA YAAHIDI KUMTUNZA RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KAMA RAIS MSTAAFU WA 5

Chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeahidi kumtunza kwa vyema Rais John Pombe Joseph Magufuli kwa heshima zote baada ya uchaguzi kuisha Oktoba 2020.



Ni suala la mheshimiwa mstaafu mtarajiwa kuamua wapi atataka kukaa iwe Chato, Geita au Dar es Salaam au popote atapoamua nchini Tanzania na serikali mpya ya CHADEMA 2020 itampatia stahiki zote kama mstaafu aliyewahii kuitumikia Tanzania katika cheo cha juu kabisa cha utumishi wa umma.

Serikali ya CHADEMA pia itamtumia kumwakilisha Rais Tundu Lissu katika shughuli za nje ya nchi pale Rais na Makamu wake watapokuwa wamebanwa, utaratibu huu wa kuwatumia wastaafu ulianza tangu enzi za wastaafu Mwalimu Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete na John Magufuli atapata wasaa wa kufanya shughuli kama mstaafu ndani na nje ya nchi.

 
Huyu Magufuli, akubali tu kutokana na wimbi kubwa la watanzania wanaotaka mabadiliko chini ya Rais mpya, shujaa Tundu Lissu, inabidi Magufuli kuanzia sasa ajiandae kisaikolojia kuwa Rais Mstaafu

Akitaka kulazimisha ushindi kwa kutumia Tume "yake" ya uchaguzi, hakika Mahakama ya kimataifa, ya The Hague, itakuwa inamuita, ili akajibu mashtaka ya "kuiba" kura za wananchi, kwenye sanduku la kura
 
Visasi havilipi ni kumuachia Mwenyezi Mungu. Nikimuangalia Lissu jinsi alivyo na furaha pamoja na udhalimu aliofanyiwa na maumivu makubwa aliyopitia yeye na familia yake kwa miaka mitatu namshukuru Mwenyezi Mungu.
 


Marais wastaafu waliomtangulia Rais John Magufuli kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kustaafu kwa heshima zote stahiki ni:
  • Julius Nyerere 1961 - 1985
  • Ali Hassan Mwinyi 1985 - 1995
  • Benjamin W. Mkapa 1995 - 2005
  • Jakaya Kikwete 2005 - 2015
 
Sio mbaya kuota ndoto! Tuwaambie tu kwamba nchi haiwezi kuendeshwa na saccos!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom