PreGE2025 CHADEMA yaendelea kupukutika, Wanachama wengine zaidi ya 100 wajivua Tabora

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kumbukeni mama kwa kipindi chake tu kakopa zaidi ya trilioni 30 so Abdul akipewa tilion moja tu ahonge watu ili wakiasi chama cha Chadema atabakiwa na chenji ya Bilioni za kutosha
 
Tunasubiri waishe kabisa tuanze kukijenga chama...wapi Boni Yai, wapi sugu?
 
Kuna dada mmoja ametaja moja ya sababu ya yeye kutoka ni ccm ukiwasusia wanakomba kila kitu na hajaona hao watanzania wa kuzuia uchaguzi.

Ina maana anachoona yeye No reform No election ni project inayoenda kufeli na haina tofauti na Chadema kususa.
 
CCM huwa wanaandaa mikutano yao kwa kubeba watu na kuhonga ili watu wajae wapate uhalali wa wizi wa kishindo kwenye "chafuzi" ili kuhalalisha "ushindi wa kishindo".

Tafiti ambayo ilifanywa na REDET mwaka 2015 ilionyesha kuwa hata kama CCM wanategemea wizi wa kura wa kishindo, kwa miaka hii (2015) na mbeleni, Watanzania wengi wanaelekea kuacha kushiriki zoezi la uchaguzi kwani kuna viashiria kuwa kura zao sio zinazotumika katika kuamua mshindi.

CCM wakaamua kuja na mbinu mpya ya kuvimaliza vyama pinzani vyenye nguvu (hasa hasa CHADEMA) kwa kuanza na kununua viongozi wake, wakiamini katika ule msemo usemao, " mpige mchunga kondoo na kondoo zitatawanyika".

Ambacho CCM walishindwa kuelewa kwenye ile tafiti ya Mkandala, ni kwamba Watanzania wa leo (2015) na miaka ijayo, sio wale wa miaka ya 80, 90 na 2000.
 
Mimi siyo CHADEMA na wala sina Chama lakini nikikumbuka msoto walioupitia tokea 2016-2020, nafikiri, hii ni cha mtoto. Kama haikufa enzi za JPM, haiwezi kufa kwa sasa. Isahavuka mengi makubwa zaidi ya hivi "vidrama"
 
CHADEMA kina mamilioni ya wanachama. .
Kuna mzee mmoja alihoji, kama CCM wanaamini wana wanachama na wafuasi wengi, kwa nini wanachukua namba za kadi za mpigakura!!??
Namba hizo wao wana kazi gani nazo!???
 
Hili ni pigo jingine kwa Chadema ya Lissu na Heche.badala ya kuvutia wanachama tunashuhudia massive exodus!!
 
Kwa mujibu wa Chadema Digital, Chadema ina wanachama zaidi ya mil 15, sasa jumlisha hao 55 akina Mrema na hao wengine, umepata ngapi?
 
Mungu mwema sana
 
Kwa mujibu wa Chadema Digital, Chadema ina wanachama zaidi ya mil 15, sasa jumlisha hao 55 akina Mrema na hao wengine, umepata ngapi?
+Ambao tulikuwa hatuna kadi
Mi ndo nataka nijiunge rasmi
Hivi Ile no ya kuchangia ni ngapi
Kwenye tone tone
 
BWANA WAOO KAPIGWAA KITU KIZITOOO

KWENTR UCHAGUZIII HAHAHAAA HAWANA HAMUUU

MIRIJAA I.MEKATAAAA
 
💪💪Mwanza Kuna Wanaume
Na hapo hujashuhudia Mara , Serengeti na Shinyangs ndugu yangu. Subiri, mambo yanakuja

Baadhi ya hao covid-55 wanadai wao ndio waliiwezesha Chadema kukubalika maenaeo hayo.

Haya tuwape fursa waende huko Na upuuzi wao huo kama hawajapondwa mawe.

NB: lSamahani, ni G-55 na si Covid-55! Naomba radhi kwa kosa hilo, halikuwa la kukusudia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…