PreGE2025 CHADEMA yaendelea kupukutika, Wanachama wengine zaidi ya 100 wajivua Tabora

PreGE2025 CHADEMA yaendelea kupukutika, Wanachama wengine zaidi ya 100 wajivua Tabora

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Jumla ya wanachama 110 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Tabora wamejivua uanachama wa chama hicho.

Miongoni mwa wanachama waliojivua uanachama ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema mkoani humo, James Kabepele.

Wanachama hao wamesema miongoni mwa sababu zilizopelekea kujivua ni pamoja ni kudharauliwa mawazo yao ndani ya chama, hawako tayari kutokushiriki uchaguzi kwani hiyo ni haki yao ya msingi.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, James Kabepele amesema baadaye watasema rasmi kuwa watajiunga na chama gani kwa sababu siasa ni maisha ni lazima waifanye.

Mapema jana, viongozi Mei 11, 2025 viongozi 58 wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Gervas Mgonja walitangaza kujivua uanachama wa chama kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho.

Viongozi wengine waliojivua ni Katibu wa Bawacha Kanda ya Kaskazini, Rachael Sadick, Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kilimanjaro, Grace Kiwelu, Mjumbe wa kamati ya Tehama Kanda ya Kaskazini, Answary Kimaro na Mwenyekiti wa Chadema mstaafu Mkoa wa Kilimanjaro, Michael Kilawila.

Jana pia kundi la makada 80 wa chama hicho Mkoa wa kichama Temeke jijini Dar es Salaam walijivua uanachama.

Chanzo: Mwananchi

haha hivi huko Heche anakopita ni lazima wawe chadema maana kuwa watu mamilioni na wanaongezeka kila siku. Hiki chama ni chama cha watanzania sio watu 100!!
 
Na hapo hujashuhudia Mara , Serengeti na Shinyangs ndugu yangu. Subiri, mambo yanakuja

Baadhi ya hao covid-55 wanadai wao ndio waliiwezesha Chadema kukubalika maenaeo hayo.

Haya tuwape fursa waende huko Na upuuzi wao huo kama hawajapondwa mawe.

NB: lSamahani, ni G-55 na si Covid-55! Naomba radhi kwa kosa hilo, halikuwa la kukusudia!
😂😂Sawa sawa
 
Acha ujinga kijana, ww na wahuni wenzako hamna ubavu wa kuitawanya CDM.
 
Back
Top Bottom