CHADEMA yafunika Mabaraza ya Tume, CCM, maelfu wajitokeza kujadili, kutoa maoni

CHADEMA yafunika Mabaraza ya Tume, CCM, maelfu wajitokeza kujadili, kutoa maoni

attachment.php

Eti wanasema tufanye mikutano ya ndani sasa ukumbi gani una weza kuingiza watu wote hawa...R.I.P CCM

Achana na wahuni hao!
Wanajua kwamba mikutano ya wazi ni kama mtego wa panya...
Hata CCM wanajua ukweli kupitia mikutano hiyo na kuwadharau sana makanjanja wao kuna Nape na Mwigulu!
 


Ndio maana kwenye uchaguzi wa 2010 mlituletea makamu wa rais wa darasa la 7? . Kweli mliwadharau watanzania

Kama darasa la saba ni elimu duni, kwa nini serikali ya magamba inawahitimisha watanzania kwa ngazi hiyo?!
Kwa hiyo mhitimu wa darasa la saba kwenu ana faida anapowapigia kura peke yake?!
 
Chezea chadema wewe,jipange' 2015 ng'adu kwa ng'adu, mpaka kieleweke, tabora mpoooooo! Badilikeni sasa!
 
Sijui mama yako alikuwa anakumbuka nini alipoamua kukuita KYAMTUNDU

Pole sana ndugu yangu NDUKA!
Kyamtundu ni jina la mahali ninakotoka ila am proud of regardless of how many interpretations will come from the ceased mindsets!
 
Ni katika uwendawazimu wa hali ya juu tu ndipo unaweza kujaribu kukubaliana na mleta mada. Yaani kama siyo kujidanganya au kwahadaa wananchi, unaweza kujadili jambo hapo? zaidi ya watu mia moja kwenye mkutano wa hadhara na wa wazi kama huo huwezi kujadili kitu sana sana ni kuhutubia, kutoa msimamo kisha kuwaambia waliojitokeza waandike maoni ambapo kiuhakika maana ni mambo ya wazi hakuna atakayethubutu narudia kwa desturi yetu hakuna atakayethubutu kuandika kinyume na matarajio ya wengi katika hadhara hiyo lazima wote waaandika kukidhi msimamo na hasa wa anayehutubia.

Eti watu wametoa maoni 3.4milion alafu yanapelekwa kwa lori hii akili au tope? (Kweli Slaa na wanaomshauri hamnazo) pamoja na kwamba chadema imeshachambua na kuyajadili mapendekezo yao katika halmashuri kuu ya chama bado yeye na wanaomshauri ameoni vyema akayapeleka makaratasi yote kwa Jaji Warioba kweli hakuona aibu hata waliokua wanazunguka naye kwenye hiyo mikutano hawakumsindikiza? Huyu rais mtarajiwa vipi? jamani mnaomshauri huyu mzee mnamdhalilisha (ndugu yangu Makene nadhani unapaswa kukumbuka ulichofundishwa na Dr. Nasro pale IJMC - Critical thinking and argumentation kisha umpe mzee wetu ushauri nasaha maana hii ni cheap popularity (kimsingi ni populist)).

Mleta mada nakushauri ujitambue alafu utambue hili ni jukwaa la critical thinkers, hivyo weka mambo yako vyema kabla hujaleta humu. Siyo kila kitu siasa ndugu jaribu kufikiria kwanza. Hii ni katiba ya Tanzania ambayo inakula kote yaani must cut across ili kila mtu afaidi hata kama ni kidogo. hamna kulinda maslahi fulani, wala si katiba wa chama fulani. Hapa mnawanyima wananchi uhuru wa kutoa maoni yao (mnabaka demokrasia ilihali ni chama cha demokrasia), toeni msimamo wa chama kisha waambieni wananchi watoe maoni. Kwenye mikutano yote iliyofanywa sijaona point ya maana zaidi ya kuiponda ccm na kuwahadaa wananchi kuwa ccm imeingilia mchakato wa katiba ili tu ionekane Kikwete hakua wala hana nia ya kuleta katiba mpya. Eti ccm hawataki tunu za taifa kwenye katiba mpya ccm hawataki serikali tatu sisi tunavitaka hivyo ili tuwabane mafisadi hao na kuingia Ikulu. hahahaaaa wasomeeni wananchi kilicho kwenye rasimu ya katiba mpya kisha mtoe kasoro yenu siyo kuing'ang'ania ccm kwani katiba ni ya ccm hiyo jamanii? Kwa mfano sijasikia kina Dr. Slaa (dr wa kanisani siyo katika elimu inayokubaliwa na katiba mpya, maana kwa aktiba mpya haitambui kama Dr. Slaa ana digrii) akizungumzia Sura ya 18 (a) inayohusu hazina na 18 (d) benki kuu. Sura ya 4 inazungumzwa sana sehemu ya kwanza inayozungumzia kaki za binadamu ila sehemu ya pili chadema hawaigusi wanasubiri waingie madarakani kisha watuambie unaona kuna upande wa pili wa shilingi maana inazungumzia (a) wajibu wa raia kwa Taifa na (b) wajibu wa mamlaka za nchi - hii nayo inazungumziwa sana hasa kwa mifano ya Mwangosi na Ulimboka nk.

Tujadili katiba siii vyama
 
Back
Top Bottom