PostGE2025 CHADEMA yailaani Serikali kwa kuizuia Tume ya Haki za Binadamu ya Bunge la Ulaya kutembelea Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani vikali uamuzi wa utawala haramu wa Samia Suluhu Hassan wa kuzuia ujumbe rasmi wa Kamati Ndogo ya Haki za Binadamu ya Bunge la Ulaya kutembelea Tanzania.

Hatua hii ni jaribio jingine la wazi la utawala huu haramu kuficha ukweli kuhusu mauaji ya tarehe 29 Oktoba 2025, pamoja na kuzuia uchunguzi huru, uwajibikaji wa kimataifa na ufuatiliaji wa haki za binadamu, wakati hali ya demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria nchini ikiendelea kuzorota kwa kasi. Serikali inayoheshimu misingi ya kidemokrasia haiogopi uwazi, uchunguzi huru wala ushirikiano na taasisi za kimataifa zinazotetea haki za binadamu na utawala wa sheria. Kukataliwa kwa ziara hii kunadhihirisha kuendelea kuimarika kwa utawala wa kimabavu nchini Tanzania unaotegemea hofu, ukandamizaji na utamaduni wa kutoadhibiwa.

Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imeshuhudia ongezeko kubwa la ukandamizaji wa kisiasa, utekaji na upotezwaji wa watu kwa nguvu, ukamataji holela, vizuizi dhidi ya wanahabari na asasi za kiraia, mashambulizi dhidi ya vyama vya upinzani, pamoja na kudhoofishwa kwa haki za kikatiba na uhuru wa kisiasa. Ukandamizaji huu umejenga mazingira ya hofu na utamaduni wa kutoadhibiwa unaokiuka misingi ya haki za binadamu na wajibu wa kimataifa ambao Tanzania imekuwa ikidai kuuheshimu.

Soma Pia: Serikali ya Tanzania yadaiwa kuwazuia Wabunge wa Ulaya (EU) Kufanya Ziara Nchini

Vitendo hivi sasa vimeongezewa uzito na kauli za hivi karibuni za Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara ya Rais wa Kenya William Samoei Ruto, ambapo alionekana kuhimiza ukandamizaji mkali dhidi ya vijana wa Gen-Z na sauti nyingine zinazopinga utawala wa mabavu. Kauli kama hizo kutoka kwa anayejiita Mkuu wa Nchi ni za hatari, zisizo za kidemokrasia, na zinazodhoofisha misingi ya haki za binadamu, utawala bora na utawala wa

SnapInsta-Ai_3893377360111734675.jpg
SnapInsta-Ai_3893377366512295937.jpg
 
View attachment 3586237View attachment 3586238
Hiyo Tume nayo ilikuwa ya Mchongo Tu waliokuja bila taarifa
 
Back
Top Bottom