Mkuu umeongea mengi ya msingi Ila nikukosoe sehemu moja tu, hili taifa halijajigawa. Kama ilivyo mitazamo ya mambo mengine mitandaoni na hili lipo hivyo. Mfano mwaka 2016,2017 nilikuwa nje ya nchi kwa muda wa miezi mingi nilikuwa nikipitia humu naogopa, nilihisi Tanzania watu hawana hata 200 ya kunywa chai asubuhi kwa namna uchumi ulivyokuwa unaongelewa humu. Kila thread ni uchumi unayumba, uchumi unayumba.Wengine njaa,njaa mpaka Lissu naye kuingiza siasa kwenye njaa.Niliporudi nikashangaa mambo tofauti kabisa, mtaani ni picha tofauti na ya humu JF. Hivyo hivyo swala unalolisema la kuligawa Taifa, kwa mtu asiyekuwa nchini angepitia Jamii Forums akaona thread zenu za kuiombea mabaya Taifa Stars na LIKES kibao angesikitika Sana akihisi watanzania wamefikia hapa?, kumbe ni wanafiki wachache tu wa mitandaoni.Nimeenda Taifa huo umati wa watu na foleni za magari, uswahilini ndo usiseme na wachache waliotaka timu ifungwe ni sababu za kubet(Mikeka), wenyewe wanasema nimeiua Taifa Stars point zilikuwa nyingi, wala hawana time na siasa zenu. Nimegundua ndo maana mmejazana humu kudanganyana eti watu wanamchukia JPM na serikali hii, mwakani mtashangazwa Sana msipobadilika. Watu sio wajinga kuzungusha tena mikono.