Chadema yaipongeza Taifa Stars kwa kufuzu AFCON 2019


Unachekesha Ile mbaya, watu wanapenda soka sio kwa itikadi zao bali watu walikereka na kitendo cha wanasiasa wa siasa majitaka kuweka kimbelembele kutaka sifa wasizostahili. Soka letu linachangamoto kibao, huko ndio nguvu za viongozi zilipaswa kuanza kuonekana, sio wasubiri dakika za mwisho kuja kutaka point za mezani pindi wanapoona mafanikio yamekaribia.

Hiyo taifa star iliyoshinda na hata ingeshindwa wapenda mpira wataendelea kupenda na wale wasiopenda watachukulia poa, ila walio wengi walitaka kuonyesha wanasiasa wanaoligawa taifa kuacha kimbelembele kwani hawana ridhaa ya umma. Hata kama taifa stars imeshinda bado ujumbe umefika kwa huyo aliyekuwa anazodolewa. Ukweli ni kuwa mchango wa serikali ni mdogo kwenye michezo, hiyo kujiweka mbele mbele sasa ni kusaka sifa wasizostahili.
 
Mkuu umeongea mengi ya msingi Ila nikukosoe sehemu moja tu, hili taifa halijajigawa. Kama ilivyo mitazamo ya mambo mengine mitandaoni na hili lipo hivyo. Mfano mwaka 2016,2017 nilikuwa nje ya nchi kwa muda wa miezi mingi nilikuwa nikipitia humu naogopa, nilihisi Tanzania watu hawana hata 200 ya kunywa chai asubuhi kwa namna uchumi ulivyokuwa unaongelewa humu. Kila thread ni uchumi unayumba, uchumi unayumba.Wengine njaa,njaa mpaka Lissu naye kuingiza siasa kwenye njaa.Niliporudi nikashangaa mambo tofauti kabisa, mtaani ni picha tofauti na ya humu JF. Hivyo hivyo swala unalolisema la kuligawa Taifa, kwa mtu asiyekuwa nchini angepitia Jamii Forums akaona thread zenu za kuiombea mabaya Taifa Stars na LIKES kibao angesikitika Sana akihisi watanzania wamefikia hapa?, kumbe ni wanafiki wachache tu wa mitandaoni.Nimeenda Taifa huo umati wa watu na foleni za magari, uswahilini ndo usiseme na wachache waliotaka timu ifungwe ni sababu za kubet(Mikeka), wenyewe wanasema nimeiua Taifa Stars point zilikuwa nyingi, wala hawana time na siasa zenu. Nimegundua ndo maana mmejazana humu kudanganyana eti watu wanamchukia JPM na serikali hii, mwakani mtashangazwa Sana msipobadilika. Watu sio wajinga kuzungusha tena mikono.
 
Rubbish jayeed
 
The silliest man at work
 
CHADEMA acheni unafiki, nyie si ndio mliokuwa mnaiombea Taifa Stars ifungwe na kumbeza Makonda Kuhamasisha Watu Waende Uwanjan? Mashetani Wakubwa Nyie
Mimi nilitaka tufungwe, ila ndo hivyo imekuwa tofauti,
 
Hivi kesi mliyomfungulia Karia imeishia wapi?mlifanya ushirikina timu ishindwe ila sasa mmeumbuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)*

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA*

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatoa pongezi kwa Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu, Taifa Stars, pamoja na makocha wao wakiongozwa na Ndugu Emmanuel Amunike, kwa ushindi mnono wa magoli 3 dhidi ya Uganda katika mechi iliyochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo ambayo sasa yanamaanisha kuwa Tanzania imefuzu na itashiriki Mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AfCON 2019) huko Misri, Taifa Stars imetutoa Watanzania wote kimasomaso na kumaliza kiu na hamu ya muda mrefu ya wapenzi wa soka, baada ya kusubiri kwa miaka 39 kupata nafasi hii tena baada ya kushiriki mashindano hayo mwaka 1980 huko Nigeria.

Ni matumaini yetu kuwa Wachezaji wa Taifa Stars na makocha wao watazichukulia pongezi hizi pamoja na furaha kubwa isiyo kifani waliyonayo Watanzania kama chachu kubwa ya hamasa itakayowapatia ari na mori wa kushindana na timu za mataifa mengine huko Misri baadae mwaka huu na kurejea na matokeo mazuri yatakayowatangaza na kuwauza wao kimataifa na kuinufaisha nchi yetu Tanzania kwa ujumla.

Hongera Taifa Stars, *Hongera CCM*, hongera Watanzania. Kila la heri Taifa Stars AfCON 2019.

*Imetolewa leo Jumapili, Machi 24, 2019 na;*

*Tumaini Makene*

*Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano*
*Chadema*
 
CHADEMA acheni unafiki, nyie si ndio mliokuwa mnaiombea Taifa Stars ifungwe na kumbeza Makonda Kuhamasisha Watu Waende Uwanjan? Mashetani Wakubwa Nyie
Ndo maana hawajampongeza Makonda kumbe walitaka tufungwe!
 
Wacha ungese wako hapa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani vijana wameliinuwa taifa wangesikiliza ujinga wa Makonda na wema sepetu eti waende na viroba vya bia uwanjani tungelala 3 0 hero vijana kwa kuuwa uzalendo na kukarabati umaamuma wa makonda
 
Mwakinyo anajitegemea binafsi sifa inapewa ccm watanzania kwa kunafiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo maana hawajampongeza Makonda kumbe walitaka tufungwe!
Makonda ha ha apongezwe kwa lipi wale vijana walisema nchi sio upuuzi wa Makonda unatangaza ulevi kweli hiyo ni akili heko Taifa stars mumeonyesha hamuendeshwi na washamba kama makonda
 
Sipendi kabisa mambo ya UCCM na UCDM ktk kila kitu na hasa siku ya jana.
Wengine tulienda kwa uzalendo na sio porojo za kisiasa, nilifurahi sana kuona Watanzania tukishikamana kwa pamoja na kufurahi pamoja.
Natamani tungekuwa tunaungana pamoja ktk mambo ya muhimu, hawa wanasiasa ni watu wanaojali maslahi yao tu, hawana uzalendo kama wanavyohubiri.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

******** afananishwe na Mwl.Nyerere itakuwa ni kituko cha karne!!
Mzee Ruksa(Rais mstahafu Mwinyi) alikataa kufananishwa na Nyerere akisema ni sawa KULINGANISHA KICHUGUU NA MLIMA KILIMANJARO!
******** hafikii hata robo ya Mzee Ruksa.....hivo kumlinganisha na Nyerere ni sawa kulinganisha Kilimanjaro na Tambarare....!!kwi..kwi...kwi!
 
Wewe hali mitaani unaiona njema sio!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiangalia nyuzi za kabla ya mechi utaona wazee wa kuitakia nchi mabaya walitaka tufungwe. Na wengine wakaahidi na mafi lakini cha kushangaza kwa unafiki saa hizi wanajikomba komba eti tuko nao pamoja. Hawa watu ni wanafiki sjapata kuona.
Ccm anzisheni timu yenu kama TOT hamjalatazwa, National team msituletee uchoko wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiangalia nyuzi za kabla ya mechi utaona wazee wa kuitakia nchi mabaya walitaka tufungwe. Na wengine wakaahidi na mafi lakini cha kushangaza kwa unafiki saa hizi wanajikomba komba tuko nao pamoja. Hawa watu ni wanafiki sjapata kuona.
Never trust CHADEMA Leo wanajifanya kusifia baada ya sala zao za ovyo kufeli ilifikia mahali wakataka watz tufarakane kisa jezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…