- Source #1
- View Source #1
wakuu
===
Nimekutana na hizi taarifa ni kweli CHADEMA watashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, mwenye taarifa za ukweli atusaidie.
===
Nimekutana na hizi taarifa ni kweli CHADEMA watashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, mwenye taarifa za ukweli atusaidie.
- Tunachokijua
- Madai
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X Julai 4, 2025 katika ukurasa wake amechapisha grafiki yenye utabulisho wa chombo cha habari cha ITV ikiwa na ujumbe unaosomeka “CHADEMA YAJIPANGA KUREJEA KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA UCHAGUZI MKUU 2025"
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kujiridhisha kuwa si ya kweli.
Ufuatiliaji umebaini hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na CHADEMA kuhusu wao kujipanga kurejea katika mchakato wa uchaguzi mkuu 2025, pia hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo.
Juni 30, 2025 Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche alizungumza ambapo pamoja na mambo memgime alisisitiza kuwa hawatoshiriki katika uchaguzi hadi pale mabadiliko yatakapofanywa katika mifumo ya uchaguzi.
Grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ikiwa na utambulisho wa ITV ni ya kughushi kwani ina baadhi ya mapungufu ikiwemo kutumia mwandiko (fonts) tofauti na unaotumiwa na chombo hicho katika grafiki zao. Mapungufu mengine ni katika tarehe, rejelea kwa upande wa mwezi grafiki ya kughushi imetumia “Jul” ikiwa grafiki halisi zinatumia “Julai”.