Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Chadema tunalaani kwa nguvu zote tukio la uvamizi uliofanywa leo tarehe 05 Septemba 2025 katika ofisi za Jamii Forums, zilizopo Mikocheni, Jijini Dar es Salaam, na watu walioidai kuwa wanatoka katika mamlaka za usalama. Tukio hili linaashiria kukandamizwa kwa uhuru wa habari, kuminya uhuru wa kujieleza, na kuhatarisha usalama wa wananchi, kinyume kabisa na misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa watu hao walidai kutaka kompyuta za ofisi pamoja na kumtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Bwana Maxence Melo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bwana Maxence Melo amethibitisha tukio hili na kueleza:
Tunatoa wito kwa:
Soma Pia: Maxence Melo: Ofisi za JamiiForums, Mikocheni zimevamiwa
Chadema tutaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa tukio hili na kutoa taarifa zaidi kadri tunavyozipata.

“Kuna uvamizi usio rafiki uliofanyika muda sio mrefu katika ofisi za Jamii Forums Mikocheni, Jijini Dar es Salaam, wakinitafuta mimi.”
Tunatoa wito kwa:
Soma Pia: Maxence Melo: Ofisi za JamiiForums, Mikocheni zimevamiwa
- Serikali na vyombo husika kutoa ufafanuzi wa haraka juu ya tukio hili na hatua zinazochukuliwa ili kulinda haki na usalama wa wahusika.
- Vyombo vya usalama kuhakikisha vinazingatia taratibu na sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ili kujenga imani kwa wananchi.
- Wananchi na wadau wa habari kusimama kidete kutetea na kulinda uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.
Chadema tutaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa tukio hili na kutoa taarifa zaidi kadri tunavyozipata.