PreGE2025 CHADEMA yamburuza Msajili wa Vyama vya Siasa Mahakamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Amekwama wapi na Kwa lipi?

Tulikubaliana hamuendi popote ,hamtaki ruzuku mna tonetone na mkafikia mbali kwamba alitaka afute chama Leo vipi mnakula uharo wenu? 😂😂😂😂
Suala sio ruzuku Chadema sio Kikundi cha wahuni kama CCM imezoea kufanya mambo shaghala baghala ni wao.
Uendeshaji wa taasisi ni zaidi ya ruzuku wewe akili zako umepeleka wapi? Kwani mkiwa chawa mnazuiwa kuhifadhi akili kidogo kuficha upumbavu wenu
 
My Take
Njaa ni mbaya sana ila Kuna nyumbu wanatumiwa kutengenezea maisha wengine.😂😂😂

Tulikubaliana tonetone inatosha ,mahakamani mnaenda kudai ruzuku ya nini Sasa?

Msiposhiriki uchaguzi itakuaje ? 😬😬😬😬👇👇

Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), John Heche amesema chama hicho kinakwenda mahakamani kwa sababu Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeamua kuzuia ruzuku ya chama hicho.

Heche ameeleza hayo leo Jumatano Juni 4,2025 wakati akisoma maazimio ya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi jana kujadili barua ya Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa.

“Sheria ya Vyama vya Siasa anayoisimamia Msajili kifungu cha 18 (6), msajili ana uwezo wa kuzuia ruzuku ya vyama au kwa chama kingine chochote pale ambapo kuna dosari ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu ya Serikali (CAG)

Soma Pia: Msajili asitisha ruzuku CHADEMA, atishia kusimamisha shughuli za chama wakiendelea kukaidi na kuwatambua viongozi

“Sasa kama tungekuwa na hati mbaya au… kwa mujibu wa kifungu cha 18 (6) hapo msajili angepata mamlaka ya kuzuia ruzuku, kwa kutuandikia barua na kuonyesha sababu,” amesema Heche.

Hata hivyo, Heche amedai Msajili ameamua kujifanyia kwa kuchukua uamuzi huo, akisema Chadema kinakwenda mahakamani kupingia hatua hiyo.
Chawa tulia, chama lenu Chaumma limejidodea Mza, pelekeni wana CCM walau wafike mikutanoni - mmefeli vby sana - backfired na wananchi mtie adabu.

Si kwa aibu ile aisee!!
 
Kwani tone tone haitoshi kuendesha chama?
Hyo ruzuku wamuachie tu CHEDEMA IPO mioyoni mwa wananchi😂
 
Hahaha walichotaka wasiojulikana nficho chadema imekifanya.
Mjue hamtochomoka humo kwenye kesi.

Kila mkigeuka mtaambiwa kesi iko mahakamani, na ya mahakamani mnayajua, hiyo ni milele.
You think you are smatter than everybodyelse
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, ametangaza kuwa chama hicho kitafungua kesi kupinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, akisema ni kinyume na sheria na demokrasia. Ametoa kauli hiyo leo Juni 4, 2025, Jijini Dar es Salaam alipowasilisha maazimio ya Kamati Kuu ya chama mbele ya waandishi wa habari.

"Tarehe 03 Juni 2025, Kamati Kuu ya chama chetu (CHADEMA) imekaa, kupokea na kujadili juu ya taarifa aliyoitoa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa umma tarehe 27 Mei 2025 ikiwa ni msingi kutoka kwenye barua aliyoiandika kwa Katibu Mkuu tarehe 12 Mei 2025, katika barua aliyoiandika kwa chama Msajili ameelekeza kwamba chama kijaze nafasi zilizo wazi za viongozi ambao awali walikuwa wameteuliwa na kuthibitishwa na Baraza Kuu la tarehe 22 Januari 2025, sambamba na Wakurugenzi wa chama ambao waliteuliwa baadaye na vikao vya chama ambao waliteuliwa baadaye na vikao vya Kamati Kuu vilivyofuatia mwezi Februari na tarehe 10 na 11 mwezi Machi 2025"

"Kamati Kuu baada ya kutafakari kwa kina imeamua kwenda Mahakamani kwa vile imeshindwa kuiona nia njema ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika maamuzi yake aliyoelekeza kwenye barua aliyoitoa kama taarifa kwa umma, Kamati Kuu imewaelekeza Wanasheria wa chama kuwa hadi kufikia Alhamisi tarehe 09 Juni 2025 shauri hili liwe limepelekwa Mahakamani"

"Kuhusu taarifa aliyoitoa Msajili wa Vyama vya Siasa ya kuzuia ruzuku ya chama (CHADEMA), tunaenda Mahakamani kwa sababu Msajili wa Vyama vya Siasa amechukua jukumu la kuzuia ruzuku ya chama chetu, sasa sheria anayoisimamia Msajili mwenyewe yaani Sheria ya Vyama Siasa, kifungu cha 18(6) kinasema Msajili ana uwezo wa kuzuia ruzuku ya chama kingine chochote cha siasa kinachopokea ruzuku pale tu ambapo kuna kweli ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa chama hicho"

"Kwamba labda chama kimefanya matumizi ya hovyo ya fedha na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) amekagua na ametoa ripoti, kama vile mnavyosikia ripoti ya CAG inasema serikali imefanya matumizi yasiyokuwa na tija, sasa kwetu sisi (CHADEMA) kama mkaguzi angekuwa amekagua tukapata hati chafu kwa mfano au fedha zimetumika vibaya, au jambo lingine lolote linalofanania na hilo, kwa mujibu wa kifungu hicho cha 18(6) hapo tu ndipo Msajili anapopata mamlaka ya kuzuia ruzuku"

"Utaratibu wa jambo hili unaenda mpaka kwenye utaratibu ikiwemo barua, na hilo linaenda mpaka kwenye Baraza la Wadhamini la chama, kwa sababu chama hiki ni mali ya Baraza la Wadhamini, sasa ili hatua hiyo ifikiwe ni lazima chama kishindwe na Bodi ishindwe, na ripoti maalum za ukaguzi zioneshe kwamba kuna matumizi ya hovyo, sasa tunaenda Mahakamani kuonesha kutokubaliana na jambo hilo"

chadema nayo wana roho kama ya hamas.kesi ya mwenyekiti bado mbichi,leo mnafungua kesi dhidi ya msajiri? kwani mkikubari mkakaa kamati kuu mkawachagua hao waliyokatliwa na msajiri mnapoteza nini ikiwa masharti yatakuwa yamezingatia? Tanzania naona tumelogwa
 
Hahaha walichotaka wasiojulikana nficho chadema imekifanya.
Mjue hamtochomoka humo kwenye kesi.

Kila mkigeuka mtaambiwa kesi iko mahakamani, na ya mahakamani mnayajua, hiyo ni milele.
Wape njia bora watakayotumia usiishie kuwananga!
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, ametangaza kuwa chama hicho kitafungua kesi kupinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, akisema ni kinyume na sheria na demokrasia. Ametoa kauli hiyo leo Juni 4, 2025, Jijini Dar es Salaam alipowasilisha maazimio ya Kamati Kuu ya chama mbele ya waandishi wa habari.

"Tarehe 03 Juni 2025, Kamati Kuu ya chama chetu (CHADEMA) imekaa, kupokea na kujadili juu ya taarifa aliyoitoa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa umma tarehe 27 Mei 2025 ikiwa ni msingi kutoka kwenye barua aliyoiandika kwa Katibu Mkuu tarehe 12 Mei 2025, katika barua aliyoiandika kwa chama Msajili ameelekeza kwamba chama kijaze nafasi zilizo wazi za viongozi ambao awali walikuwa wameteuliwa na kuthibitishwa na Baraza Kuu la tarehe 22 Januari 2025, sambamba na Wakurugenzi wa chama ambao waliteuliwa baadaye na vikao vya chama ambao waliteuliwa baadaye na vikao vya Kamati Kuu vilivyofuatia mwezi Februari na tarehe 10 na 11 mwezi Machi 2025"

"Kamati Kuu baada ya kutafakari kwa kina imeamua kwenda Mahakamani kwa vile imeshindwa kuiona nia njema ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika maamuzi yake aliyoelekeza kwenye barua aliyoitoa kama taarifa kwa umma, Kamati Kuu imewaelekeza Wanasheria wa chama kuwa hadi kufikia Alhamisi tarehe 09 Juni 2025 shauri hili liwe limepelekwa Mahakamani"

"Kuhusu taarifa aliyoitoa Msajili wa Vyama vya Siasa ya kuzuia ruzuku ya chama (CHADEMA), tunaenda Mahakamani kwa sababu Msajili wa Vyama vya Siasa amechukua jukumu la kuzuia ruzuku ya chama chetu, sasa sheria anayoisimamia Msajili mwenyewe yaani Sheria ya Vyama Siasa, kifungu cha 18(6) kinasema Msajili ana uwezo wa kuzuia ruzuku ya chama kingine chochote cha siasa kinachopokea ruzuku pale tu ambapo kuna kweli ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa chama hicho"

"Kwamba labda chama kimefanya matumizi ya hovyo ya fedha na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) amekagua na ametoa ripoti, kama vile mnavyosikia ripoti ya CAG inasema serikali imefanya matumizi yasiyokuwa na tija, sasa kwetu sisi (CHADEMA) kama mkaguzi angekuwa amekagua tukapata hati chafu kwa mfano au fedha zimetumika vibaya, au jambo lingine lolote linalofanania na hilo, kwa mujibu wa kifungu hicho cha 18(6) hapo tu ndipo Msajili anapopata mamlaka ya kuzuia ruzuku"

"Utaratibu wa jambo hili unaenda mpaka kwenye utaratibu ikiwemo barua, na hilo linaenda mpaka kwenye Baraza la Wadhamini la chama, kwa sababu chama hiki ni mali ya Baraza la Wadhamini, sasa ili hatua hiyo ifikiwe ni lazima chama kishindwe na Bodi ishindwe, na ripoti maalum za ukaguzi zioneshe kwamba kuna matumizi ya hovyo, sasa tunaenda Mahakamani kuonesha kutokubaliana na jambo hilo"

Mwanzo walisema hawautambui uamuzi wa Msajili eti hana mamlaka na kwamba wataendelea kuwatambua viongozi wao walioteuliwa Januari!! Imekuwaje tena sasa wametambua kuwa Msajili ni baba lao au?. Nyumbu ni shida sana.
 
kwani kuna ugumu gani mkirudia na kuweka data sawa? Sioni sababu ya kwenda mahakamani ni kupoteza muda
Tatizo watu hamjui Chadema inataka nini nchi hii, Chadema wanajua mawakili anawaonea! Kwahiyo wakimwendekeza atazidi kuwaombea haha katika mambo mengine!

Kwahiyo,Ili kuondoa uonevu kwao na kwa vyama vingine, walishinda kesi ,wanakua wameweka msingi ,ambao mahakama ,au kesi nyingine zitafanya marejeo,kwamba, rejea kesi ya Chadema na msajili, kuhusu kufutwa kwa Viongozi wa Chadema walioteuliwa na vikao halali vya Chama, maamuzi ya mahakama yalikua A,B,C wanataka ku set precedent. Ili maonevu kama haya yasirudiwe tena nchini!
 
Back
Top Bottom