- Source #1
- View Source #1
Wakuu hii Taarifa una uhalisia kiasi gani?
- Tunachokijua
- Mange Kimambi ni mwanaharakati ambaye amekuwa akitoa matamko mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii kuhusu hali ya kisiasa na mambo mengine yanayoendelea nchini Tanzania.
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na barua inayosambaa yenye utambulisho wa Chama cha demokrasia na maendeleo na kudaiwa kuwa imesainiwa na Katibu mkuu wa Chama hicho John Mnyika.
Barua hiyo ina ujumbe unaeleza kumuonya mwanaharakati Mange Kimambi kuhusu matamko yake na kuwataka Watanzania wampuuze.
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa barua hiyo ni ya kubuni na haijachapishwa wala kutolewa na chama hicho kupitia mitamdao yake ya kijamii ikiwemo Instagram.
Barua hiyo pia ina baadhi ya dosari ikiwemo kutumia anwani tofauti na inayotumiwa na CHADEMA, anwani ya kwenye barua ya kubuni insaomeka,
"Nyumba Na 170
Mtaa wa Ufipa, Kinondoni
S.L.P 31191
Dar es salaam, Tanzania"
Kwa sasa anwani ya chama hicho inayotumika ikiwemo kwenye taarifa zao kwa Umma za hivi karibuni ni,
"Nyumba Na. 31
Mtaa wa Daima, Mikocheni
S.L.P 31191
Dar es salaam, Tanzania"