Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , kimetoa muda wa siku 3 kuanzia leo hadi 13/4/2023 kwa Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa awe amewajibika kutoka na ubadhirifu wa kutisha ambao umeanikwa na ripoti ya CAG .
Kauli hii ya kikakamavu imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye makao makuu ya chama hicho huko Kinondoni , Nje ya Jiji la Dar es Salaam .
Mnyika amesema kwamba ubadhirifu huu ni Ushahidi wa wazi kabisa wa uwajibikaji mbovu wa Waziri Mkuu , ambaye ndiye Mtendaji Mkuu , mdhibiti mkuu na msimamizi mkuu wa utekezaji wa shughuli zote za Serikali .
Mnyika amedai kwamba ripoti ya CAG kwa miaka 2 sasa imeonyesha madudu mengi mno yasiyo na majibu , huku kukiwa hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa , na katika kipindi chote hicho Msimamizi wa Shughuli za Serikali , kwa maana ya Waziri Mkuu ni Kasimu Majaliwa .
Chadema inatarajia Waziri Mkuu atatumia hotuba ya kuidhinisha bajeti ya ofisi yake tarehe 13/4/2023 bungeni Dodoma kutangaza pia kujiuzulu baada ya kushindwa kabisa kusimamia shughuli za serikali kama kiapo chake kinavyomuelekeza .
Mungu ibariki Tanzania .