CHADEMA yampa siku tatu Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa awe amewajibika

CHADEMA yampa siku tatu Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa awe amewajibika

Hawa Chadema naona bora wangechukua muda mrefu zaidi waje na ripoti kamili, kuliko hivi walivyofanya kutoa ripoti nusu, sijui walikuwa na haraka ya nini kufanya hivi, njoo na jambo kamili, uki-push, una push moja kwa moja.

Sio leo wenasema PM na Mwigulu wanapaswa kujiuzulu, kesho tena wakija na nusu ripoti iliyobaki waseme fulani na fulani wanatakiwa kujiuzulu, wakati hawa wa mwanzo bado wako ofisini, mwishowe unageuka usanii mtupu.
Wanawawahi ACT Wazalendo
 
Mimi napitia uchambuzi wa ACT Wazalendo hapa!
Nakuona hapo
IMG-20230410-WA0046.jpg
 
View attachment 2583352

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , kimetoa muda wa siku 3 kuanzia leo hadi 13/4/2023 kwa Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa awe amewajibika kutoka na ubadhirifu wa kutisha ambao umeanikwa na ripoti ya CAG .

Kauli hii ya kikakamavu imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye makao makuu ya chama hicho huko Kinondoni , Nje ya Jiji la Dar es Salaam .

Mnyika amesema kwamba ubadhirifu huu ni Ushahidi wa wazi kabisa wa uwajibikaji mbovu wa Waziri Mkuu , ambaye ndiye Mtendaji Mkuu , mdhibiti mkuu na msimamizi mkuu wa utekezaji wa shughuli zote za Serikali .

Mnyika amedai kwamba ripoti ya CAG kwa miaka 2 sasa imeonyesha madudu mengi mno yasiyo na majibu , huku kukiwa hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa , na katika kipindi chote hicho Msimamizi wa Shughuli za Serikali , kwa maana ya Waziri Mkuu ni Kasimu Majaliwa .

Chadema inatarajia Waziri Mkuu atatumia hotuba ya kuidhinisha bajeti ya ofisi yake tarehe 13/4/2023 bungeni Dodoma kutangaza pia kujiuzulu baada ya kushindwa kabisa kusimamia shughuli za serikali kama kiapo chake kinavyomuelekeza .

Mungu ibariki Tanzania .
Huu ndo ujinga WA wapinzani wetu
 
Sasa Chadema mmeona mkimsema samia mtakuwa mmetibua asali bora mmeseme Majaliwa hahahaha

Sasa Majaliwa ana kosa gani?
Kama Samia anawogopa mawaziri na wakuu wa taasisi nani atawawajibisha?

Chadema mna vichekesho sana….mmeshindwa ata kusema waziri fulani ajiuzulu?
 
chadema hawezi kumuajibisha hata muuza mboga sokoni itakuwa waziri mkuu
 
Sasa Chadema mmeona mkimsema samia mtakuwa mmetibua asali bora mmeseme Majaliwa hahahaha

Sasa Majaliwa ana kosa gani?
Kama Samia anawogopa mawaziri na wakuu wa taasisi nani atawawajibisha?

Chadema mna vichekesho sana….mmeshindwa ata kusema waziri fulani ajiuzulu?
Hivi Majukumu ya waziri mkuu ni yapi ?
 
Naona Ukinzani na hili jambo.....nisiseme sana, picha inajieleza....Unafikiri Mzee wetu J.MK anatuhabarisha nini hapa
fb_img_1680258242993-jpg.2572153
 
Back
Top Bottom