CHADEMA yampa siku tatu Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa awe amewajibika

View attachment 2583352

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , kimetoa muda wa siku 3 kuanzia leo hadi 13/4/2023 kwa Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa awe amewajibika kutoka na ubadhirifu wa kutisha ambao umeanikwa na ripoti ya CAG .

Kauli hii ya kikakamavu imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye makao makuu ya chama hicho huko Kinondoni , Nje ya Jiji la Dar es Salaam .

Mnyika amesema kwamba ubadhirifu huu ni Ushahidi wa wazi kabisa wa uwajibikaji mbovu wa Waziri Mkuu , ambaye ndiye Mtendaji Mkuu , mdhibiti mkuu na msimamizi mkuu wa utekezaji wa shughuli zote za Serikali .

Mnyika amedai kwamba ripoti ya CAG kwa miaka 2 sasa imeonyesha madudu mengi mno yasiyo na majibu , huku kukiwa hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa , na katika kipindi chote hicho Msimamizi wa Shughuli za Serikali , kwa maana ya Waziri Mkuu ni Kasimu Majaliwa .

Chadema inatarajia Waziri Mkuu atatumia hotuba ya kuidhinisha bajeti ya ofisi yake tarehe 13/4/2023 bungeni Dodoma kutangaza pia kujiuzulu baada ya kushindwa kabisa kusimamia shughuli za serikali kama kiapo chake kinavyomuelekeza .

Mungu ibariki Tanzania .
Kwa.nini Chadema wanashindwa kusema Rais Samia Suluhu ndiye anahitajika kujiuzuri? Timu ikishindwa kuleta matokeo chanya, anaondolewa kocha sio captain wa timu..
 
View attachment 2583352

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , kimetoa muda wa siku 3 kuanzia leo hadi 13/4/2023 kwa Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa awe amewajibika kutoka na ubadhirifu wa kutisha ambao umeanikwa na ripoti ya CAG .

Kauli hii ya kikakamavu imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye makao makuu ya chama hicho huko Kinondoni , Nje ya Jiji la Dar es Salaam .

Mnyika amesema kwamba ubadhirifu huu ni Ushahidi wa wazi kabisa wa uwajibikaji mbovu wa Waziri Mkuu , ambaye ndiye Mtendaji Mkuu , mdhibiti mkuu na msimamizi mkuu wa utekezaji wa shughuli zote za Serikali .

Mnyika amedai kwamba ripoti ya CAG kwa miaka 2 sasa imeonyesha madudu mengi mno yasiyo na majibu , huku kukiwa hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa , na katika kipindi chote hicho Msimamizi wa Shughuli za Serikali , kwa maana ya Waziri Mkuu ni Kasimu Majaliwa .

Chadema inatarajia Waziri Mkuu atatumia hotuba ya kuidhinisha bajeti ya ofisi yake tarehe 13/4/2023 bungeni Dodoma kutangaza pia kujiuzulu baada ya kushindwa kabisa kusimamia shughuli za serikali kama kiapo chake kinavyomuelekeza .

Mungu ibariki Tanzania .
Mwamsheni Mnyika mwambieni atoke usingizini anafanya matumizi mabaya ya usingizi
 
Sasa Chadema mmeona mkimsema samia mtakuwa mmetibua asali bora mmeseme Majaliwa hahahaha

Sasa Majaliwa ana kosa gani?
Kama Samia anawogopa mawaziri na wakuu wa taasisi nani atawawajibisha?

Chadema mna vichekesho sana….mmeshindwa ata kusema waziri fulani ajiuzulu?

nimeanza kukuelewa kaka!
 
Akijiuzulu Waziri Mkuu, ndiyo mwisho wa baraza lote la mawaziri.

Nielimishe kwanini PM ajiuzulu wakati Tayari Makatibu wakuu na Wakurugenzi wamepewa Kazi ya Kupitia ripoti?
 
Kuna mpuuzi mmoja anadai chadema walipewa pesa ili wasiongelee mambo ya TANESCO ameshupaza shingo sijua kwamba hata kula amekula leo

Alisema Dkt. Mollel:

FpojyuNWIAAJNp3.jpeg
 
Hawa Chadema naona bora wangechukua muda mrefu zaidi waje na ripoti kamili, kuliko hivi walivyofanya kutoa ripoti nusu, sijui walikuwa na haraka ya nini kufanya hivi, njoo na jambo kamili, uki-push, una push moja kwa moja.

Sio leo wenasema PM na Mwigulu wanapaswa kujiuzulu, kesho tena wakija na nusu ripoti iliyobaki waseme fulani na fulani wanatakiwa kujiuzulu, wakati hawa wa mwanzo bado wako ofisini, mwishowe unageuka usanii mtupu.

Presentation ni art.

Nadhani pana haja ya kuwachagua vyema wasilisha mada.

Tunahitaji watu wa ku maintain momentum. Tunawahitaji kina Raila. Hao wapo. Tuwatumie.

Suala la chief strategist si suala la kupuuzia.

Siasa ni sayansi.
 
Kwani umeshindwa kuzitambua hoja za Chadema au za Prof. Assad hapo?

Au ni kile kizungu zungu Cha siku zote ukipatacho kila usikiapo jina Chadema?
Hoja ya Chadema ni kwanini Halima Mdee na Mama Kaboyoka walikaa pembeni ya CAG Kichere mmoja upande wa kushoto na mwingine mkono wa kulia!!!
 
View attachment 2583352

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , kimetoa muda wa siku 3 kuanzia leo hadi 13/4/2023 kwa Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa awe amewajibika kutoka na ubadhirifu wa kutisha ambao umeanikwa na ripoti ya CAG .

Kauli hii ya kikakamavu imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye makao makuu ya chama hicho huko Kinondoni , Nje ya Jiji la Dar es Salaam .

Mnyika amesema kwamba ubadhirifu huu ni Ushahidi wa wazi kabisa wa uwajibikaji mbovu wa Waziri Mkuu , ambaye ndiye Mtendaji Mkuu , mdhibiti mkuu na msimamizi mkuu wa utekezaji wa shughuli zote za Serikali .

Mnyika amedai kwamba ripoti ya CAG kwa miaka 2 sasa imeonyesha madudu mengi mno yasiyo na majibu , huku kukiwa hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa , na katika kipindi chote hicho Msimamizi wa Shughuli za Serikali , kwa maana ya Waziri Mkuu ni Kasimu Majaliwa .

Chadema inatarajia Waziri Mkuu atatumia hotuba ya kuidhinisha bajeti ya ofisi yake tarehe 13/4/2023 bungeni Dodoma kutangaza pia kujiuzulu baada ya kushindwa kabisa kusimamia shughuli za serikali kama kiapo chake kinavyomuelekeza .

Mungu ibariki Tanzania .
Haiwezi kutumbuliwa sababu ni muumini
 
Back
Top Bottom