CHADEMA yampa siku tatu Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa awe amewajibika

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , kimetoa muda wa siku 3 kuanzia leo hadi 13/4/2023 kwa Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa awe amewajibika kutoka na ubadhirifu wa kutisha ambao umeanikwa na ripoti ya CAG .

Kauli hii ya kikakamavu imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye makao makuu ya chama hicho huko Kinondoni , Nje ya Jiji la Dar es Salaam .

Mnyika amesema kwamba ubadhirifu huu ni Ushahidi wa wazi kabisa wa uwajibikaji mbovu wa Waziri Mkuu , ambaye ndiye Mtendaji Mkuu , mdhibiti mkuu na msimamizi mkuu wa utekezaji wa shughuli zote za Serikali .

Mnyika amedai kwamba ripoti ya CAG kwa miaka 2 sasa imeonyesha madudu mengi mno yasiyo na majibu , huku kukiwa hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa , na katika kipindi chote hicho Msimamizi wa Shughuli za Serikali , kwa maana ya Waziri Mkuu ni Kasimu Majaliwa .

Chadema inatarajia Waziri Mkuu atatumia hotuba ya kuidhinisha bajeti ya ofisi yake tarehe 13/4/2023 bungeni Dodoma kutangaza pia kujiuzulu baada ya kushindwa kabisa kusimamia shughuli za serikali kama kiapo chake kinavyomuelekeza .

Mungu ibariki Tanzania .
 
Uzuri wa CHADEMA haina papara.. Maana kuna wajinga walishaanza kuongea
 
Mkuu sometimes mnazingua yaan mnajua fika hakunaga utaratib wa kuwajibika viongoz ndan ya utawala wa CCM!! Sa mnatoa amri kwa Mr kessy 🤣🤣🤣🤣
 
Chadema wanataka PM ajiuzulu wakiwa na maana kwamba wameridhishwa na utendaji kazi wa Rais?

Bahati nzuri huyu Mnyika ndie aliwahi kumuita JK dhaifu, hebu atuambie, mpaka sasa hajaona viashiria vyovyote vya udhaifu kwa huyu aliyepo?

Anyway, ngoja kwanza niweke kiporo maoni mengine nikiwasubiri wamalizie huo uchambuzi wao, siku wakimalizia kiporo kilichobaki naamini nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutia neno katika hili.
 
Ripoti ya CAG iko wazi kuhusu wizi na utendaji mbovu uliotufikisha huku.

Wanaotufikisha kwenye wizi na ubadhirifu huu wanajulikana. Ya nini basi kuendelea kuandikia mate?









Bila kufurushwa watu hawa, utamaduni binafsi wa kuwajibika wenyewe haupo.

Hii ni hata kama wakiitwa "stupid people" hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…