CHADEMA yampa siku tatu Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa awe amewajibika

CHADEMA yampa siku tatu Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa awe amewajibika

Na wenyewe ni yale yale tu wapigaji, kama hawawezi kujua kiasi walichopata kwenye kampain yao ya join the chain watatuambia nini kuhusu ufisadi? Yaani hii nchi sina imani na wanasiasa kutoka chama chochote kile.
 
Na wenyewe ni yale yale tu wapigaji, kama hawawezi kujua kiasi walichopata kwenye kampain yao ya join the chain watatuambia nini kuhusu ufisadi? Yaani hii nchi sina imani na wanasiasa kutoka chama chochote kile.
jikite kwenye mada
 
Chadema wanataka PM ajiuzulu wakiwa na maana kwamba wameridhishwa na utendaji kazi wa Rais?

Bahati nzuri huyu Mnyika ndie aliwahi kumuita JK dhaifu, hebu atuambie, mpaka sasa hajaona viashiria vyovyote vya udhaifu kwa huyu aliyepo?

Anyway, ngoja kwanza niweke kiporo maoni mengine nikiwasubiri wamalizie huo uchambuzi wao, siku wakimalizia kiporo kilichobaki naamini nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutia neno katika hili.
Yaani mwamba unatoa madini Sana sikuwahi kukufikiria
 
View attachment 2583352

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , kimetoa muda wa siku 3 kuanzia leo hadi 13/4/2023 kwa Waziri Mkuu Mh Kasimu Majaliwa awe amewajibika kutoka na ubadhirifu wa kutisha ambao umeanikwa na ripoti ya CAG .

Kauli hii ya kikakamavu imetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye makao makuu ya chama hicho huko Kinondoni , Nje ya Jiji la Dar es Salaam .

Mnyika amesema kwamba ubadhirifu huu ni Ushahidi wa wazi kabisa wa uwajibikaji mbovu wa Waziri Mkuu , ambaye ndiye Mtendaji Mkuu , mdhibiti mkuu na msimamizi mkuu wa utekezaji wa shughuli zote za Serikali .

Mnyika amedai kwamba ripoti ya CAG kwa miaka 2 sasa imeonyesha madudu mengi mno yasiyo na majibu , huku kukiwa hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa , na katika kipindi chote hicho Msimamizi wa Shughuli za Serikali , kwa maana ya Waziri Mkuu ni Kasimu Majaliwa .

Chadema inatarajia Waziri Mkuu atatumia hotuba ya kuidhinisha bajeti ya ofisi yake tarehe 13/4/2023 bungeni Dodoma kutangaza pia kujiuzulu baada ya kushindwa kabisa kusimamia shughuli za serikali kama kiapo chake kinavyomuelekeza .

Mungu ibariki Tanzania .
Hii ilishia wapi sijui
 
Back
Top Bottom