CHADEMA yampongeza Rais mpya wa Zambia, Hakainde Hichilema kwa ushindi wa kishindo

Historia

Mlolongo wa njama chafu za Edgar Lungu na chama chake hatimaye zafikia tamati :

14 Juni 2021

Kampeni za H.H mwezi Juni 2021


 
Historia

Mlolongo wa njama chafu za Edgar Lungu na chama chake hatimaye zafikia tamati :

14 Juni 2021

Kampeni za H.H mwezi Juni 2021


kushinda uchaguzi ni kitu kimoja, kutekeleza ni swala lingine
 
Hivi ndoto za Chadema miaka 20 bado mnaendelea kuota tu. Wenzenu wameamka wananchi wanawaamini, nyie bado mnaota tu. Mtaishia kuota tu na kufanya ugaidi.
 
Haiwezi kutoa nafuu yoyote kwa chadema,Huo ni utamaduni wa Zambia sawa tuu na Malawi,Ghana,Kenya na Botswana.

Huku Tzn utaratibu ni chama dola na si vinginevyo.
 
Fursa zipi sasa, kwani nyie lengo la chama chenu ni nn?
Lengo la chama chetu ni kuona fursa zinatolewa kwa usawa,mfano mdogo Gwajima anapingana na msimamo wa rais wake na chama chake,imetolewa amri ya kukamatwa Jeshi la polisi wamesema lazima kuwe nyaraka halali ili wamkamate,kwa mpinzani ikitamkwa tu mara moja jeshi la polisi linatekeleza mapema sana
 
Si kweli. CHAMA DOLA ndio adui wa wapenda haki na maendeleo duniani kote. Ni tatizo zaidi ya corona (rejea Lipumba).
na kwa nini mpinzani naye akiingia tu madarakani anakuwa kama aliyetoka maana baada ya muda tu kidoigo naye lawama za upinzani zinamgeukia yeye?
 

gwajima, polisi,.. skuelewi! ebu semeni msimamo ulio nyooka
 
gwajima, polisi,.. skuelewi! ebu semeni msimamo ulio nyooka
Pili uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu ni vielelezo tosha,vile vile wale wabunge wa viti maalum ambao inasemekana ni wabunge waliotokana na Chadema na chadema kupitia kikao halali na nyaraka halali kiliwafuta uanachama,lakini serikali ya ccm ikatumia nguvu kuwalinda kuwa ni wabunge wa chadema,ina maana chadema kama chama halali hawana maamuzi yao mpaka yaingiliwe na ccm?
Au kwa vile chadema hawana dola ndiyo maana ccm inatumia mwanya huo kuvuruga mambo makusudi ambayo ni jinai hapo baadaye?Unapowashambulia chadema uwashambulie kwa sababu za msingi na sio ushabiki na dharau ambazo baadaye zitakuja kuumiza baadhi ya watu,weka kumbukumbu.
 
na kwa nini mpinzani naye akiingia tu madarakani anakuwa kama aliyetoka maana baada ya muda tu kidoigo naye lawama za upinzani zinamgeukia yeye?
Mpinzani akiingia madarakani si mpinzani tena ni mtawala. Anapimwa kama chama tawala. Anatolewa maana akionyesha mwenendo mbovu wa kukiuka haki za binadamu na kupuuza katiba, sheria. Anakaliwa kimya akifanya mazuri kama anavyotarajiwa.

Kiuhalisia kuna vyama mbadala tu. Anayeingia madarakani anakuwa chama tawala na anayejikuta nje anakuwa upinzani (opposition) akiwa na jukumu la kuu la kukosoa chama tawala na serikali yake wasipofanya vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…