- Source #1
- View Source #1
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Heche, amesema kuwa chama hicho kiko tayari kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, endapo Tume ya Uchaguzi itawapa nafasi hiyo.
- Tunachokijua
- John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Mnamo tarehe 12 Aprili 2025 CHADEMA ilitoa msimamo wake kuhusu kikao cha kusaini maadili kanuni za maadili ya uchaguzi na kutokushiriki kusaini kwa kanuni hizo na kwamba msimamo huo ulitokana na kutokuwepo kwa majibu ya maandishi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu barua rasmi iliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika Desemba 29, 2024 akieleza mapendekezo na madai ya msingi ya CHADEMA kuhusu mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na kueleza kuwa ukimya huo ulithibitisha kukosekana kwa nia ya dhati ya kufanya mashauriano ya kweli na ya wazi kuhusu mchakato wa uchaguzi.
Aidha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X John Heche alisisitiza msimamo huo kwa kusema hawawezi kusaini maadili ya tume isiyo na maadili.
"Chama chetu hakitashiriki kusaini maadili ya tume isiyo na maadili. Tume kupitia watumishi wake inashiriki kuiba kura, wanawaengua wagombea wetu kwa uongo, wanahujumu na kuzuia mawakala wetu kuingia kwenye vituo. Hakuna maadili ya kusaini kwa watu wasio na maadili."
Kumekuwapo na Chapisho linalosambazwa mitandaoni likidaiwa kuchapishwa na Jambo TV likiwa na kichwa cha habari, Heche asema 'tunaomba tume itupe nafasi ya kushiriki uchaguzi mkuu'
Je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (KeWorSearch), imebainika kuwa Taarifa hiyo Si ya Kweli, ni ya kutengenezwa kwani haikuchapishwa katika kurasa zao rasmi za Jambo TV.
Aidha kupitia mkutano na waandishi wa Habari Heche aliwaalika wananchi kwenda Makamani Kisutu kwenda kusikiliza kesi ya uhaini inayomhusu Tundu Lissu iliyokuwa imepangwa kufanyika Aprili 24, 2025 pia alitumia nafasi hiyo kueleza namna alivyozuiwa kufanya mkutano wa hadhara eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam.