TANZIA CHADEMA yapata pigo Dodoma, Kamanda Tully Nassa Kiwanga afariki dunia

TANZIA CHADEMA yapata pigo Dodoma, Kamanda Tully Nassa Kiwanga afariki dunia

Nilipokuwa katika Msafara wa Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu kuna wakati niliugua njiani. Wakati Msafara ulipokuwa ukielekea Kongwa mimi na watu wengine wawili tulitangulia Dodoma Mjini. Wakati tumkisubiri Shehe Ponda kuja kuungana nasi, nilipelekwa pamoja na Mangwesh katika Ofisi za CHADEMA ili kujiangalizia!
Hapo ndipo nilipotambulishwa kwa Tully Kiwanga na wengine. Alijitahidi sana kutuhudumia mimi na Mangwesh lakini niliishia kunywa maziwa tu kwa kuwa hali yangu ya kiafya haikuniruhusu kula chakula wakati ule!

Nilimuona Tully kama binti mcheshi na mwenye uthubutu mwingi sana. Alifurahia sana kuniona nimefika Ofisini kwao!

Leo nimeambiwa na Mheshimiwa Magrateth Mugyabuso kuwa Tully amefarakana na dunia hii na kuyaaga rasmi maisha haya! Nilitarajia kumuona Tully mjini Dodoma wakati mimi na Timu yangu tunakwenda kuongoza "Matembezi ya Hiyari"! Hakika! Sutakuona tena Tully! Umeondoka kabla macho yako hayajashuhudia haki ile ambayo tumekuwa tukiipambania! Mungu anayejihusisha sana na masuala ya haki akizikumbuke kazi zako!

Ninatoa pole sana kwa familia, CHADEMA Kanda ya Kati, ndugu, jamaa, marafiki na wale wote walioguswa na msiba huu!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 
kumpiga picha hivyo kama kapanua miguu akiwa kama anasubiri mwanaume ampande juu nini hicho ? hapo ni hospitali au guest house ? picha ya kidhalilishaji hiyo itoe
Unaona akili yako ilivyo ya kitoto sawa na ya panzi au pimbi.Hujaombwa ufafanue au uelezee insha ya picha.Tafsiri ya hiyo picha unapewa taarifa rasmi hali halisi za hosipitali zetu zilivyo.Na ugonjwa unaoendelea kwa sababu wewe unajaribu kutupotosha kwa kutueleza mambo ya kijinga na kuthubutu kuandika hivyo na wewe utaandikwa tena ndugu zako hawataamini macho yao.Wee subiri tu.Ni tahadhari unapewa.1.Angalia mazingara ya hosipitali,angalia kitanda,angalia shuka na vitu vingine ujue tunakoelekea sivyo.Nadhani wakati wako utakuwa umetandikiwa ngozi ya mbuzi kwenye kitanda cha spring.Hiyo ni tahadhari kuwa "WANATUDANGANYA KUWA JAMAA HAYUPO NCHINI,MWENYE MACHO HAPA ANAAMBIWA TAZAMA AU ONA.Fikiria kabla hujaandika mjinga wewe.
 
Siyo kila anayewekewa ventilation ana corona.
Jipe moyo.Tembea pekupeku kila mahali.Umesikia ee usiache.Endelea kuwasikiliza hao wajinga wenzako.Hakuna atakayeangaika na familia yako itakayobaki.Pumzika kwa amani.Umepigania vizuri kutafuta haki na demokrasia kwa Watanzania.Tutaienzi juhudi yako.RIP
 
hivi kwanini wanaccm wanawaza ngono tu , tena style ya kishamba ya kifo cha mende ?
Ndivyo walivyo.Na uwaelewe hivyo.Kila mahali.Hata hapa kwetu yupo mmoja.Yaani ukisikia mawazo yake.Utaona aibu huyu mtu ametokea wapi.Ni pumba tupu.
 
Unaona akili yako ilivyo ya kitoto sawa na ya panzi au pimbi.Hujaombwa ufafanue au uelezee insha ya picha.Tafsiri ya hiyo picha unapewa taarifa rasmi hali halisi za hosipitali zetu zilivyo.Na ugonjwa unaoendelea kwa sababu wewe unajaribu kutupotosha kwa kutueleza mambo ya kijinga na kuthubutu kuandika hivyo na wewe utaandikwa tena ndugu zako hawataamini macho yao.Wee subiri tu.Ni tahadhari unapewa.1.Angalia mazingara ya hosipitali,angalia kitanda,angalia shuka na vitu vingine ujue tunakoelekea sivyo.Nadhani wakati wako utakuwa umetandikiwa ngozi ya mbuzi kwenye kitanda cha spring.Hiyo ni tahadhari kuwa "WANATUDANGANYA KUWA JAMAA HAYUPO NCHINI,MWENYE MACHO HAPA ANAAMBIWA TAZAMA AU ONA.Fikiria kabla hujaandika mjinga wewe.
Msamehe bure manake na sisi hatujui miisho yetu itakuwaje!?
tuna viburi na kejeli kwasababu tunapumua.
 
Apumzike kwa amani

View attachment 1698315View attachment 1698316

Lakini kwa vile kufanya kazi ya Chadema ni sawa na kutenda kazi ya Mungu , tunaamini Mwenyezi Mungu ataipokea roho yake mahali pema peponi , Amina .
Tafadhali mpe heshima stahiki marehemu. Siyo kila kitu unaweka siasa zako za maji taka. Please be mature. Mungu ampe pumziko la amani dada Tully aliyelala.
 
Back
Top Bottom