Elections 2010 CHADEMA Yapeta Mpanda mjini; Yarudisha majimbo yake yote except 1!!

Elections 2010 CHADEMA Yapeta Mpanda mjini; Yarudisha majimbo yake yote except 1!!

Ok poa ila wanaweza kutuachia hata haya majimbo mawili,ni majimbo mawili tunaongoza ingawa moja ndo confirmed tuko juu zaidi
 
Msimamizi wa uchaguzi ameishatangaza tayari kuwa Mpanda Mjini wamechukua Chadema, na Mpanda Vijijini wamechukua CCM. TBC wametangaza asubuhi kwenye Jambo Tanzania.
 
Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz!!!!!!!!!!!!!!!!

Poweeeeeeeeeeeeeeerrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
mgombea wa ccm ubunge mpanda mjini anaitwa kapufi kama sijakosea jina lake , ni mchimba madini pale mpanda anaubia na waarabu kuchimba dhahabu katika migodi yake.pongezi chadema kuendelea kulishikilia hilo jimbo.
vipi kuhusu yule mgombea udiwani ccm mpanda mjini anaitwa william mbogo ?aliridhi mali za ukoo ikiwemo migodi ya dhahabu pale mpanda, je ameshinda udiwani?mwenye habari atuhabarishe.
 
MGOMBEA wa ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jimbo la Mpanda Mjini, Said Arfi anaongoza katika jimbo hilo katika vituo 27 kati ya vituo 28 vilivyokuwa vimetangaza matokeo ya kura ya ubunge mpaka jana jioni wakati vituo vyote ni 104.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimemsimamisha Sebastian Kapufi, katika vituo hivyo kilikuwa kikiongoza katika kituo kimoja tu cha Rasko, ambako mgombea wake
alipata kura 65 na kufuatiwa kwa karibu na Arfi aliyepata kura 61 huku mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Ndimumenya Ezekye akiambulia sifuri katika vituo hivyo.

Jumla ya vituo ni katika vituo vingine na kura za wagombea katika mabano ni Azimio 1, Chadema (124), CCM (23), Azimio 2, Chadema (72), CCM (62), Azimio 3 Chadema (88), CCM (49), Azimio 4, Chadema (72), CCM (55), Azimio 5, Chadema (72), CCM (62).

Katika kituo cha Paradise 1, Chadema (64), CCM (62), Paradise 2, Chadema (94), CCM (55), Paradise 3, Chadema (100), CCM (68), Paradise 4, Chadema (94), CCM (63), Majengo Chadema (73), CCM (65), Makanyagio 1, Chadema (64), CCM (63), Makanyagio 2, Chadema (86), CCM (59).

Makanyagio 3, Chadema (103), CCM (73), Makanyagio 4, Chadema (92), CCM (64), Makanyagio 5, Chadema (88), CCM (69), Isikama 1, Chadema (90), CCM (67), Isikama 2, Chadema (108), CCM (78), Isikama 3, Chadema (90), CCM (73).

Wakati wa kupiga kura mashabiki wa CCM na Chadema, walionesha wasiwasi mkubwa kutokana na mahudhurio hafifu ya watu waliojitokeza kupiga kura karibu katika vituo vyote wakidai kuwa kasoro hiyo inaweza kuathiri matarajiwa yao.

Charles Kalifumu ambaye alidai kuwa mkeretwa na mfuasi wa CCM ambaye alipiga kura yake kituo cha shule ya msingi Mpanda alisema: “Nimeshuhudia chaguzi kadhaa maishani mwangu kwame sijaona hali kama hii hasa kwenye kituo hiki hapa cha
Paradise ambacho daima kinakuwa na misururu mirefu.

Hata hivyo, Dikson Kashula alionyesha furaha yake pamoja na vijana wengine wakidai kuwa kutojitokeza kwa akina mama kupiga kura kunaipa nafasi kubwa ya ushindi Chadema kwani vijana wengi walipiga kura asubuhi na mapema mara tu baada ya vituo kufunguliwa kwani wanadai vijana hao waliweza kujihimu vituoni kwa kuwa walikesha wanadaka kumbikumbi mitaani.

Katika jimbo la Mpanda Mjini wanaowania nafasi ya ubunge ni Said Arfi wa Chadema anayetetea nafasi hiyo kwa muhula mwingine, Sebastian kapufi wa CCM na Ndimumenya Ezekye wa CUF ambaye hajawahi kuhutubia mikutano yoyote ile kampeni kwa kile anachodai kuwa anfahamika sana kuliko mgombea yeyote.
 
Tangu CDM imeanzishwa haijawahi kuhusishwa na udini. Tatizo ni viongozi wa kikristu walipoamua kumpa sapoti Padri mwenzao kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Ukisema viongozi wa kikristo unajumuisha wakristo wote ni bora ungekuwa speciffic ni viongozi wapi?

Kwa mifano, michache tu Mikoa mingi yenye wakristo wengi ilimpa kura Kikwete badala ya Dr Slaa na baadhi ya maeneo kama Mpanda mjini na bukoba mjini Waislamu wapepata kura nyingi za wakristo na waislamu. Tusipandikize udini kwa manufaa yetu.
 
mabaki ya walewale akina 'hoja ya nguvu'
 
Tangu CDM imeanzishwa haijawahi kuhusishwa na udini. Tatizo ni viongozi wa kikristu walipoamua kumpa sapoti Padri mwenzao kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Ujinga huu pia umesemwa sana na viongozi wenu wa chama cha majambazi. Kama viongozi wa kikristo wangefanya unachokisema hapa unadhani huyo JK wenu angeshinda? Acheni ujinga. Angalia majimbo yenye wakatoliki wengi kama Peramho(95 per cent catholics) mbona wamemchagua JK kwa asilimia 76? Mnapenda sana kujenga udini nyie watu wa chama cha majambazi.
 
Katika jimbo la Mpanda Mjini wanaowania nafasi ya ubunge ni Said Arfi wa Chadema anayetetea nafasi hiyo kwa muhula mwingine, Sebastian kapufi wa CCM na Ndimumenya Ezekye wa CUF ambaye hajawahi kuhutubia mikutano yoyote ile kampeni kwa kile anachodai kuwa anfahamika sana kuliko mgombea yeyote.

Huyu jamaa kiboko!! jina lake kama la kule vile?:smile-big::smile-big:
 
chedema tuhakikishieni kuwa mh. Arf kashatangazwa na tume ya uchaguzi ili tuwahi tusker baridi
 
Back
Top Bottom