MGOMBEA wa ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jimbo la Mpanda Mjini, Said Arfi anaongoza katika jimbo hilo katika vituo 27 kati ya vituo 28 vilivyokuwa vimetangaza matokeo ya kura ya ubunge mpaka jana jioni wakati vituo vyote ni 104.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimemsimamisha Sebastian Kapufi, katika vituo hivyo kilikuwa kikiongoza katika kituo kimoja tu cha Rasko, ambako mgombea wake
alipata kura 65 na kufuatiwa kwa karibu na Arfi aliyepata kura 61 huku mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Ndimumenya Ezekye akiambulia sifuri katika vituo hivyo.
Jumla ya vituo ni katika vituo vingine na kura za wagombea katika mabano ni Azimio 1, Chadema (124), CCM (23), Azimio 2, Chadema (72), CCM (62), Azimio 3 Chadema (88), CCM (49), Azimio 4, Chadema (72), CCM (55), Azimio 5, Chadema (72), CCM (62).
Katika kituo cha Paradise 1, Chadema (64), CCM (62), Paradise 2, Chadema (94), CCM (55), Paradise 3, Chadema (100), CCM (68), Paradise 4, Chadema (94), CCM (63), Majengo Chadema (73), CCM (65), Makanyagio 1, Chadema (64), CCM (63), Makanyagio 2, Chadema (86), CCM (59).
Makanyagio 3, Chadema (103), CCM (73), Makanyagio 4, Chadema (92), CCM (64), Makanyagio 5, Chadema (88), CCM (69), Isikama 1, Chadema (90), CCM (67), Isikama 2, Chadema (108), CCM (78), Isikama 3, Chadema (90), CCM (73).
Wakati wa kupiga kura mashabiki wa CCM na Chadema, walionesha wasiwasi mkubwa kutokana na mahudhurio hafifu ya watu waliojitokeza kupiga kura karibu katika vituo vyote wakidai kuwa kasoro hiyo inaweza kuathiri matarajiwa yao.
Charles Kalifumu ambaye alidai kuwa mkeretwa na mfuasi wa CCM ambaye alipiga kura yake kituo cha shule ya msingi Mpanda alisema: Nimeshuhudia chaguzi kadhaa maishani mwangu kwame sijaona hali kama hii hasa kwenye kituo hiki hapa cha
Paradise ambacho daima kinakuwa na misururu mirefu.
Hata hivyo, Dikson Kashula alionyesha furaha yake pamoja na vijana wengine wakidai kuwa kutojitokeza kwa akina mama kupiga kura kunaipa nafasi kubwa ya ushindi Chadema kwani vijana wengi walipiga kura asubuhi na mapema mara tu baada ya vituo kufunguliwa kwani wanadai vijana hao waliweza kujihimu vituoni kwa kuwa walikesha wanadaka kumbikumbi mitaani.
Katika jimbo la Mpanda Mjini wanaowania nafasi ya ubunge ni Said Arfi wa Chadema anayetetea nafasi hiyo kwa muhula mwingine, Sebastian kapufi wa CCM na Ndimumenya Ezekye wa CUF ambaye hajawahi kuhutubia mikutano yoyote ile kampeni kwa kile anachodai kuwa anfahamika sana kuliko mgombea yeyote.