Chadema imewapiga marufuku maelfu ya watanzania ambao wana elimu ya msingi na kidato cha nne wasigombee uongozi wowote katila chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Chama hicho, japo kimewanyima haki ya kugombea, kinatarajia kwenda kuwaomba kura ili kuwatumia kisiasa kwa faida yao
Ni nadra sana kukutana na mjumbe wa serikali ya mtaa au kitongoji mwenye elimu ya kidato cha sita, achilia mbali mwenyekiti wa mtaa na wa kijiji.
Sasa ni zamu ya watanzania hao kuwaadhibu chadema kwa dhambi hii ya ubaguzi
Chama hicho, japo kimewanyima haki ya kugombea, kinatarajia kwenda kuwaomba kura ili kuwatumia kisiasa kwa faida yao
Ni nadra sana kukutana na mjumbe wa serikali ya mtaa au kitongoji mwenye elimu ya kidato cha sita, achilia mbali mwenyekiti wa mtaa na wa kijiji.
Sasa ni zamu ya watanzania hao kuwaadhibu chadema kwa dhambi hii ya ubaguzi
- Tunachokijua
- Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni mchakato wa kidemokrasia ambapo wananchi hupiga kura kila baada ya miaka mitano kuwachagua viongozi wa ngazi za mitaa kama vile Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, na Wajumbe wa Serikali za Mitaa.
Kumekuwa na barua inayosambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa ni ya CHADEMA ambayo ikionekana kuandikwa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na mambo ya nje CHADEMA, John Mrema, Barua hiyo inaeleza kuwa CHADEMA wametoa kanuni mpya ambayo inaeleza mtu anayeruhusiwa kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ni yule mwenye Elimu ya kuanzia kidato cha Sita huku barua hiyo ikiwataka Wananchi kuzingatia kanuni hiyo.
Je, Ukweli wa barua hiyo ni upi?
JamiiCheck Imefatilia taarifa zilizotolewa kwenye barua hiyo na kubaini kuwa hazina Ukweli wowote, aidha barua hiyo haijawahi kutolewa na CHADEMA kupitia kurasa zao Rasmi za mitandao ya kijamii wala kwenye vyombo rasmi vya taarifa vya CHADEMA.
Vilevile, barua hiyo haijawahi kuchapishwa kwenye akaunti za John Mrema ingawa ndiye aliyedaiwa kusaini Barua hiyo, Aidha, John Mrema amechapisha taarifa ya kanusho kupitia kaunti yake ya mtandao wa X na kueleza kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na kuwataka watu kuipuuza.
Siku za hivi karibuni viongozi mbalimbali wa CHADEMA wamekuwa wakizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, ila hawajawahi kueleza kuhusu mabadiliko ya kanuni inayowataka watu wanaotaka kugombea wawe na Elimu kuanzia kidato cha Sita na kueendela, ila wamekuwa wakisisitiza watu kwenda kujiandikisha kwa ajili ya zoezi la kupiga kura na kujiandaa kwa uchaguzi ikiwemo kujiandaa kuchagua viongozi na kuchaguliwa kuwa kiongozi na si kueleza mabadiliko ya kanuni kama barua ile ilivyoeleza.