SI KWELI CHADEMA yapiga marufuku ambao hawana elimu ya kidato cha sita na kuendelea kugombea serikali za mitaa na uchaguzi mkuu

SI KWELI CHADEMA yapiga marufuku ambao hawana elimu ya kidato cha sita na kuendelea kugombea serikali za mitaa na uchaguzi mkuu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Chadema imewapiga marufuku maelfu ya watanzania ambao wana elimu ya msingi na kidato cha nne wasigombee uongozi wowote katila chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Chama hicho, japo kimewanyima haki ya kugombea, kinatarajia kwenda kuwaomba kura ili kuwatumia kisiasa kwa faida yao

Ni nadra sana kukutana na mjumbe wa serikali ya mtaa au kitongoji mwenye elimu ya kidato cha sita, achilia mbali mwenyekiti wa mtaa na wa kijiji.

Sasa ni zamu ya watanzania hao kuwaadhibu chadema kwa dhambi hii ya ubaguzi

barua chadema.jpg
 
Tunachokijua
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni mchakato wa kidemokrasia ambapo wananchi hupiga kura kila baada ya miaka mitano kuwachagua viongozi wa ngazi za mitaa kama vile Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, na Wajumbe wa Serikali za Mitaa.

Kumekuwa na barua inayosambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa ni ya CHADEMA ambayo ikionekana kuandikwa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na mambo ya nje CHADEMA, John Mrema, Barua hiyo inaeleza kuwa CHADEMA wametoa kanuni mpya ambayo inaeleza mtu anayeruhusiwa kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ni yule mwenye Elimu ya kuanzia kidato cha Sita huku barua hiyo ikiwataka Wananchi kuzingatia kanuni hiyo.

Je, Ukweli wa barua hiyo ni upi?
JamiiCheck Imefatilia taarifa zilizotolewa kwenye barua hiyo na kubaini kuwa hazina Ukweli wowote, aidha barua hiyo haijawahi kutolewa na CHADEMA kupitia kurasa zao Rasmi za mitandao ya kijamii wala kwenye vyombo rasmi vya taarifa vya CHADEMA.

Vilevile, barua hiyo haijawahi kuchapishwa kwenye akaunti za John Mrema ingawa ndiye aliyedaiwa kusaini Barua hiyo, Aidha, John Mrema amechapisha taarifa ya kanusho kupitia kaunti yake ya mtandao wa X na kueleza kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na kuwataka watu kuipuuza.

Siku za hivi karibuni viongozi mbalimbali wa CHADEMA wamekuwa wakizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, ila hawajawahi kueleza kuhusu mabadiliko ya kanuni inayowataka watu wanaotaka kugombea wawe na Elimu kuanzia kidato cha Sita na kueendela, ila wamekuwa wakisisitiza watu kwenda kujiandikisha kwa ajili ya zoezi la kupiga kura na kujiandaa kwa uchaguzi ikiwemo kujiandaa kuchagua viongozi na kuchaguliwa kuwa kiongozi na si kueleza mabadiliko ya kanuni kama barua ile ilivyoeleza.
Pamoja na shule zote hizi za kata upatikanaji wa form four kuongoza vijiji na mitaa bado ni changamoto??

Mkuu huu ndo ukweli labda Kama haujapata nafasi ya kutembea Maeneo mengi ya vijijini .

Then kwa nafasi ya Mwenyekiti wa kitongoji swala la umri pia huwa linatazamwa pia.

Hivyo kumpta MTU mwenye 40 yrs aliyefika form six itakuwa kazi ngumu kwa vijijini .

Kigezo cha umri sio lazima Ila nimeongelea kwa uzoefu tu kuwa watu hupenda kuchagua viongozi wenye kuanzia umri huo hasa hizi nafasi za chini za Ku-deal na wanananchi moja kwa moja.
 
Kiongozi, for the sake of mjadala (ingawa nahisi tangazo ni fake) soma Ibara ya 30(2)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, halafu urudi tujadili vizuri zaidi. Hii ibara ina'restrict' haki zote zilizotolewa kwenye Katiba. Si unajua the Bill of Rights kwenye Katiba yetu "is not entrenched?" Anyway, cheki kwanza, halafu uone je Tume ikisema hivyo, itakuwa imekosea/imevunja Katiba?
Nilieleza awali kwamba kuna habari hii ni fake news.

The abstract question is still interesting.

This is essentially the question of the unconstitutionality of refusing private candidacy. The constitution allows, the election commission doesn't, simple logic dictates the election commission/law are unconstitutional and therefore invalid.

The tricky part here is that while in the case of private candidates all Tanzanians are denied that right, forcing them to join parties in order to run for office, therefore making the unconstitutionality of that requirement clear, the educational requirement of one party does not force a Tanzanian to meet that requirement, since that Tanzanian can join another party, or stary her own, and not face that requirement.

30 (2) f has no relevance here.

In fact if you must invoke 30 (2) f, it is easier to invoke it to strike down this educationalr equirement, rendering it unconstitutional.

One can say kuiminya demokrasia iliyohakikishwa na katiba kwa kuiwekea vigezo vya ziada vya kielimu si kustawisha taifa, ni kugawanya na kudumaza taifa.

Imagine tukisema kigezo minimum cha kupiga kura (si kupigiwa kura tu) ni elimu ya form six.

Hapo demokrasia haitakuwa imeminywa?

Sasa kama kigezo kitaminya demokrasia kwa wapiga kura, kwa nini kisiminye demokrasia hivyo hivyo kwa wapigiwa kura?

Tatizo ketu kubwa si katiba mbovu, tatizo letu hata mazuri yaliyo kwenye hii katiba mbovu hatuyatumii. Hatuna utamaduni wa kufuata katiba.

Ndiyo maana Magufuli aliweza kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya hadhara, jambo ambalo si tu ni haki ya kikatiba, bali pia ni haki ya kibinadamu iliyomo katika mikataba ya kimataifa tuliyoisaini na kui domesticate kwa sheria zetu nchini.


30. Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu

(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya–

(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;

(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya umma;

(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai au la jinai;

(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au maisha binafsi ya watu wanohusika katika mashauri mahakamani; kuzuia kutoa habari za siri; kutunza heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;

(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji, uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya watu binafsi nchini; au

(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.
 
Yaani utokee ugomvi wa wana ndoa mtaani mtu aupeleke kwa kijana ambaye hata hajaoa, na muda wote kalewa visungura. Mwenyekiti wa mtaa ni mzee wa busara wa eneo hilo
Hilo ni miongoni mwa majukumu ya mwenyekiti wa mtaa??😀
 
Kama ni kweli, Uamuzi wa CHADEMA kuzuia watu wasio na elimu ya kidato cha sita kugombea nafasi za uongozi wa serikali za vijiji na mitaa utaleta athari mbalimbali katika jamii ya Kitanzania, hasa kwa kuzingatia hali ya elimu na miundombinu ya kiuchumi ya nchi. Kutakuwa na madhara ya sera hii kwa chama kuelekea ushindani wake na CCM.

Tanzania bado ina idadi kubwa ya wananchi ambao hawajamaliza elimu ya sekondari kidato cha sita hasa maeneo ya vijijini. Uamuzi huu umetafsiriwa kama kujitenga kwa CHADEMA na kundi kubwa la wapiga kura ambao wanawakilishwa na watu wasio na elimu ya kidato cha sita. Kuzuia kundi hili kugombea ni kuwadharau, hali ambayo inaweza kupunguza hamasa yao ya kushiriki siasa za CHADEMA, na wataacha kuunga mkono chama hicho.

Elimu ya kidato cha sita si kigezo cha uwezo wa uongozi. Mara nyingi, uongozi bora unatokana na ujuzi wa kijamii, uzoefu wa kimaisha, na uwezo wa kuhamasisha watu katika jamii. Kwa kuweka kigezo hiki cha elimu, CHADEMA inakosa wagombea wenye uelewa mzuri wa changamoto za kijamii na kiuchumi za vijiji na mitaa ambao wanatokana na mazingira hayo, hata kama hawana elimu ya juu. Hii itaathiri ubora wa wagombea wanaotokana na chama hicho.

vijana wengi nchini Tanzania wanakabiliwa na changamoto za kumaliza elimu ya sekondari kidato cha sita kutokana na matatizo ya kiuchumi. Uamuzi wa kuwatenga vijana hawa utawakatisha tamaa, hali inayoweza kuathiri malengo ya chama ya kuhamasisha kizazi kipya kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa. Ushindani dhidi ya CCM hautakuwepo maana CHADEMA itapoteza kundi kubwa la vijana ambao ni tegemeo katika kuongeza nguvu za chama.

Demokrasia inahusisha kushirikisha watu wote, bila kujali hali zao za kiuchumi au kielimu. Kwa kuweka kigezo hiki, CHADEMA imedhoofisha taswira yake kama chama kinachopigania demokrasia shirikishi. Hii inawapa CCM fursa ya kujionyesha kama chama kinachothamini zaidi michango ya watu wa ngazi zote katika jamii, jambo ambalo huipa CCM nguvu zaidi katika ushindani wa kisiasa.

Sio lazima kuwa na elimu ya juu ili kuwa kiongozi bora. Kuna mifano mingi ya watu ambao, licha ya kutokuwa na elimu rasmi ya juu, wameweza kuwa viongozi wa mfano katika jamii zao kwa sababu ya hekima na uzoefu wa maisha. CHADEMA inapoteza wagombea wenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika vijiji na mitaa, kwa sababu tu hawana cheti cha kidato cha sita, hali itakayodhoofisha ushindani wa chama dhidi ya CCM, hasa katika maeneo ya vijijini.

Kwa kumalizia, haya ya CHADEMA inaweza kuonekana kama ni hatua inayolenga kuimarisha viwango vya elimu katika uongozi, lakini ina hatari ya kupunguza mvuto wa chama hicho kwa wapiga kura wa kawaida, vijana, na watu wenye ujuzi wa kiasili lakini wasio na elimu ya kidato cha sita. Ni maamuzi ya kibaguzi na yanayoonyesha CHADEMA haijui lolote kuhusu hali halisi ya maisha ya jamii wanayotaka kuiongoza.
CCM ni chama cha wote na kimbilio la wananchi. Huwezi kukuta ubaguzi wa hivi kwa CCM. vijana na wagombea wote waliobaguliwa na CHADEMA kwa sababu tu hamna vyeti vya Kidato cha sita, na mna sifa za kuongoza, gombeeni kupitia CCM ili kwa pamoja tumshinde huyu adui wa umma anayeleta ubaguzi wa kielimu. Sikupaswa kuwaambia CHADEMA juu ya hili kwa sababu linasaidia kuwafanya wakose uungwaji mkono. Nimesema kama ONYO kwa siasa na sera za ubaguzi wa kielimu. Huwezi kuwabagua watu wengi namna hii na mimi nikakaa kimya!
 
Nyerere alipo sema ujinga kuwa sehemu ya maadui wa taifa,alikuwa sahihi sana,wajinga ni janga kwa taifa.
 
Wananchi kokusa elimu ndio mtaji wa sisiemu kwa wajinga kuongoza wajinga, wote lazima watumbukie shimoni, naona CHADEMA wako sawa
 
chadema wanataka anguko kubwa kwakuanza kubaguana ,mkianza kubaguana hiyo ni laana wanaitafuta na watu wanatwakimbia wote
 
Kama ni kweli, Uamuzi wa CHADEMA kuzuia watu wasio na elimu ya kidato cha sita kugombea nafasi za uongozi wa serikali wakose uungwaji mkono. Nimesema kama ONYO kwa siasa na sera za ubaguzi wa kielimu. Huwezi kuwabagua watu wengi namna hii na mimi nikakaa kimya!
UJINGA NI MTAJI WA CCM
 
Yaleyaleee, nyuzi mpya deile...

Mimi sio mwanasiasa wala mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, na wala sio social scientist bali nipo kwenye natural sciences. Kwa mujibu wa research nazofanya mojawapo ni qualitative ambayo haihitaji empirical data, tunapata conclusions kwa human perceptions, feelings, thoughts, says, mitazamo, mazungumzo, reactions, nk nk.

Kwa ujumla utafiti wangu usio rasmi qualitatively, naona Chadema ni lidude moja kubwa mno na linalotisha sana kwa kutazama namna reactions, na qualitative data zilizopo humu JF, radioni, social media zingine, TV, blogs, Polisi, jeshini, mitaani, magengeni, chats, groups za chawas etc. hamna siku chadema haijatajwa mara 10 hadi 20! Kuanzia mama yao/yetu akilala, akiamka, akiongea, akiwaza, chadema inazunguka kichwani kwake, makondeko kule kwa landrover kila akiamka, makalai kwenye mizunguko yake ya perdiem, joni nchambi, tulizo kule dom, mcheza kiduku wa daslam, hapi, mkumbwa, cc yote ya ccm, machawa wazoefu na wapya kote mitandaoni, mwashamba, talalalah, choicevariable, yohana mbatizaji, na wengine lukuki. Polisi ndio wakisikia kuanzia kaka yao mkubwa anayevaa official dress na buti hata kwenye sherehe ikulu kama yupo vitani ndio wanapagawa kabisa na kuitana nchi nzima, na kuwasha mazimamoto yao ya kipigaji. Hili dude linawatisha sana kisaikolijia.

My conclusion kwa haya naona chadema sasa niifananishe na maji kwa kweli, yani ni lazima uyatumie tu ili uishi, kuna watu kwa kuitajataja tu wamepata uwaziri, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa, ubunge, uchawa rasmi, ukatibu-kata na uenezi wa ccm, wengine wakapigwa na pesa, wengine ubalozi, wengine ucovid-19 sasa hii si sawa na maji tu wandugu??

Yani utake usitake utayanywa, usipoyanywa utayaoga, usipoyaoga utafulia, usipoyafulia utapikia, usipopikia utaoshea hata tongotongo. Ili tumbo lako lisitirike kwa sasa we andika, taja, waza, ongea kuhusu chadema, ukiongelea mwengine unafutika tu kama upepo. Relavance yako itakuja kwa kusema chademaaaaa, chademaaaa hata kama huna logic km mwashamba.

Yani kuna watu wasipotaja chadema wanapotea so ili wawe relevant lazima kila siku waje na uzi kuhusu chadema tu, gosh!! Wengine hata spelling hawajui lkn chadema ipo midomoni mwao kutwa kucha.

No offence hii ni perception ya jamii ya watanzania kuanzia mama yetu shuka chini hadi kwa machawa wa level za chini kbs kama hapa nilipo cholesamvula.
 
Tayari Jamiicheki wameshakuambia SI KWELI, wajinga wajinga kama wewe mnauharibu huu mtandao kwa kuleta habari za kipuuzi
Wewe umeona Chadema wamekanusha? Au hao jamii cheki wamenukuu kiongozi yoyote wa Chadema? Au wao ni wasemaji wa Chadema?
 
Wewe umeona Chadema wamekanusha? Au hao jamii cheki wamenukuu kiongozi yoyote wa Chadema? Au wao ni wasemaji wa Chadema?
Mimi nimeona Kiongozi wa Chadema John Mrema kakanusha, Pia JamiiCheck hawakurupuki mpaka wanasem ni uongo tayari wamefatilia na kujihakikishia hilo, tazama taarifa zao.

Ila kwa kuwa wewe umezoea uongo,

Tazama hii

1728557046585.png

 
Mnaharibu sifa ya huu mtandao na ninawasifu kwa kuanzisha hii Jamiicheck
 
Back
Top Bottom