SI KWELI CHADEMA yapiga marufuku ambao hawana elimu ya kidato cha sita na kuendelea kugombea serikali za mitaa na uchaguzi mkuu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Chadema imewapiga marufuku maelfu ya watanzania ambao wana elimu ya msingi na kidato cha nne wasigombee uongozi wowote katila chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Chama hicho, japo kimewanyima haki ya kugombea, kinatarajia kwenda kuwaomba kura ili kuwatumia kisiasa kwa faida yao

Ni nadra sana kukutana na mjumbe wa serikali ya mtaa au kitongoji mwenye elimu ya kidato cha sita, achilia mbali mwenyekiti wa mtaa na wa kijiji.

Sasa ni zamu ya watanzania hao kuwaadhibu chadema kwa dhambi hii ya ubaguzi

barua chadema.jpg
 
Tunachokijua
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni mchakato wa kidemokrasia ambapo wananchi hupiga kura kila baada ya miaka mitano kuwachagua viongozi wa ngazi za mitaa kama vile Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, na Wajumbe wa Serikali za Mitaa.

Kumekuwa na barua inayosambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa ni ya CHADEMA ambayo ikionekana kuandikwa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na mambo ya nje CHADEMA, John Mrema, Barua hiyo inaeleza kuwa CHADEMA wametoa kanuni mpya ambayo inaeleza mtu anayeruhusiwa kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ni yule mwenye Elimu ya kuanzia kidato cha Sita huku barua hiyo ikiwataka Wananchi kuzingatia kanuni hiyo.

Je, Ukweli wa barua hiyo ni upi?
JamiiCheck Imefatilia taarifa zilizotolewa kwenye barua hiyo na kubaini kuwa hazina Ukweli wowote, aidha barua hiyo haijawahi kutolewa na CHADEMA kupitia kurasa zao Rasmi za mitandao ya kijamii wala kwenye vyombo rasmi vya taarifa vya CHADEMA.

Vilevile, barua hiyo haijawahi kuchapishwa kwenye akaunti za John Mrema ingawa ndiye aliyedaiwa kusaini Barua hiyo, Aidha, John Mrema amechapisha taarifa ya kanusho kupitia kaunti yake ya mtandao wa X na kueleza kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na kuwataka watu kuipuuza.

Siku za hivi karibuni viongozi mbalimbali wa CHADEMA wamekuwa wakizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, ila hawajawahi kueleza kuhusu mabadiliko ya kanuni inayowataka watu wanaotaka kugombea wawe na Elimu kuanzia kidato cha Sita na kueendela, ila wamekuwa wakisisitiza watu kwenda kujiandikisha kwa ajili ya zoezi la kupiga kura na kujiandaa kwa uchaguzi ikiwemo kujiandaa kuchagua viongozi na kuchaguliwa kuwa kiongozi na si kueleza mabadiliko ya kanuni kama barua ile ilivyoeleza.
Barua ina makosa mengi ila kwanza tuanze na hiyo saini! Saini ya Mrema! Nk digital signature au hand signature!??
 
Chadema imewapiga marufuku maelfu ya watanzania ambao wana elimu ya msingi na kidato cha nne wasigombee uongozi wowote katila chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Chama hicho, japo kimewanyima haki ya kugombea, kinatarajia kwenda kuwaomba kura ili kuwatumia kisiasa kwa faida yao

Ni nadra sana kukutana na mjumbe wa serikali ya mtaa au kitongoji mwenye elimu ya kidato cha sita, achilia mbali mwenyekiti wa mtaa na wa kijiji.

Sasa ni zamu ya watanzania hao kuwaadhibu chadema kwa dhambi hii ya ubaguzi
View attachment 3120101
C HADEMA wanajichimbia kaburi alafu waaze kuilalamikia tume ya uchaguzi wakishakula za uso.
 
Kwanza ni kinyume na Katiba na Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kuna vitu havihitaji katiba kubadilshwa ni chama husika kimya kimya kinateua mgombea msomi aliyesoma form six kimya kimya bila kumwambia huyo wa darasa la saba au form four kuwa tumekukataa sababu huna cheti cha form six

Sio kila kitu lazima kisubiri katiba mpya

Kwa hili Chadema wako sahihi kama mchungaji Mtikila alibadilisha mambo mengi kwa katiba hii hiip

Hilo halihitaji katiba kubadilishwa vyama vyenyewe vyaweza tuletea wagombea wasomi sio hao darasa la saba sababu wao ndio waidhinishaji nani agombee

Hakuna haja hata ya kubadili katiba kwenye hili vyama vya siasa vijiongeze iwe CCM au upinzani

Sio kila kitu kinahitaji katiba ya nchi ibadilishwe hata kama inasomeka darasa la saba aweza gombea serikali ya mtaa ,udiwani nk
 
Ingawa kwenye siasa kuna watu wana ushawishi mitaani bila kuwa na elimu kubwa ila nawaunga mkono CHADEMA kwenye huu uamuzi kama ni kweli. Tunahitaji wasomi wengi kwenye siasa. Mimi ningeshauri wasitoe fomu kwa form six ambaye hana ONE au TWO.
 
Chadema imewapiga marufuku maelfu ya watanzania ambao wana elimu ya msingi na kidato cha nne wasigombee uongozi wowote katila chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Chama hicho, japo kimewanyima haki ya kugombea, kinatarajia kwenda kuwaomba kura ili kuwatumia kisiasa kwa faida yao

Ni nadra sana kukutana na mjumbe wa serikali ya mtaa au kitongoji mwenye elimu ya kidato cha sita, achilia mbali mwenyekiti wa mtaa na wa kijiji.

Sasa ni zamu ya watanzania hao kuwaadhibu chadema kwa dhambi hii ya ubaguzi
View attachment 3120101
Hii ni kutaka kumpindua Mh.Mbowe kabisa...tukatae ili mapema iwezekanavyo
 
Chadema wako makini sana kuandaa viongozi.Hawataki mambumbumbu kama ilivyo ccm
 
  • Dislike
Reactions: UCD
Kuna vitu havihitaji katiba kubadilshwa ni chama husika kimya kimya kinateua mgombea msomi aliyesoma form six kimya kimya bila kumwambia huyo wa darasa la saba au form four kuwa tumekukataa sababu huna cheti cha form six

Sio kila kitu lazima kisubiri katiba mpya

Kwa hili Chadema wako sahihi kama mchungaji Mtikila alibadilisha mambo mengi kwa katiba hii hiip

Hilo halihitaji katiba kubadilishwa vyama vyenyewe vyaweza tuletea wagombea wasomi sio hao darasa la saba sababu wao ndio waidhinishaji nani agombee

Hakuna haja hata ya kubadili katiba kwenye hili vyama vya siasa vijiongeze iwe CCM au upinzani

Sio kila kitu kinahitaji katiba ya nchi ibadilishwe hata kama inasomeka darasa la saba aweza gombea serikali ya mtaa ,udiwani nk
Kama barua hii ni ya kweli basi hawafanya kimya kimya kama ulivyoeleza hapo juu. Madhara yake ni kuwa kama Mwanachama wa Chadema akaamua kuomba nafasi ya kuteuliwa kugombea na wakamnyima kwa kigezo cha barua hii basi akienda Mahakamani atawashinda.
 
Mwenyekiti WA Kijiji au mtaa - kidato cha sita
Diwani- diploma au degree
Ubunge- Masters up to Phd.
Urais - PhD ya kusomea.

Chadema mko vizuri! Kuongozwa na vilaza sasa iwe mwisho.
 
Ingawa kwenye siasa kuna watu wana ushawishi mitaani bila kuwa na elimu kubwa ila nawaunga mkono CHADEMA kwenye huu uamuzi kama ni kweli. Tunahitaji wasomi wengi kwenye siasa. Mimi ningeshauri wasitoe fomu kwa form six ambaye hana ONE au TWO.
😁😁😁 wewe jamaa unaleta masihala
 
Yaani utokee ugomvi wa wana ndoa mtaani mtu aupeleke kwa kijana ambaye hata hajaoa, na muda wote kalewa visungura. Mwenyekiti wa mtaa ni mzee wa busara wa eneo hilo
Sasa ugomvi wa ndoa upeleke mwenyekiti kufanya Nini huko nako ni kukosa elimu hivi mfano wewe mmeo kakunyima uboo utamwambiaje mwenyekiti?
 
Chadema wako makini sana kuandaa viongozi.Hawataki mambumbumbu kama ilivyo ccm
Akili yako inakutuma kuwa mtu yoyote ambaye hakufika Kidato cha sita ni mbumbumbu!!?
 
Kwa nafasi ya mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa mtaa na vijiji Mara nyingi sio rahisi umpate mwenye Elimu ya Six achilia mbali form four.

Hasa vijijini .

Hii taarifa itakuwa sio rasmi. Ebu tusubiri tuone.
 
Akili yako inakutuma kuwa mtu yoyote ambaye hakufika Kidato cha sita ni mbumbumbu!!?
Hapana.kwa Ccm hata kama ana PhD ataendelea kuwa mbumbumbu tu.Si unaona Nchi walivyoihatibu?
 
Back
Top Bottom