CHADEMA yashtushwa na Fredrick Sumaye kutumia nembo ya Taifa kuitisha mkutano wake na Wanahabari

Barua imesema ofisi ya waziri mkuu mstaafu sasa wanashtuka nini kutumika nembo ya taifa. Au ofisi ya waziri mkuu ni mali ya chama hivyo inapaswa itumie nembo ya chama? Na kuzungumzia uchaguzi wa Chadema siyo kosa, labda yeye Sumaye kaamua atoe maoni kama waziri mkuu mstaafu na siyo kama mwanachadema na ndio maana katumia nembo ya taifa.
Wenyewe ndio wameona bonge la point [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
huyu ni waziri Mkuu Mstaafu na ana ofisi na Katibu wake ambaye pia analipwa na serikali so kutumia Nembo ya Serikali kwake ni sahihi kabisa. wanaojua itifaki watatuambia zaidi
 
Barua imesema ofisi ya waziri mkuu mstaafu sasa wanashtuka nini kutumika nembo ya taifa. Au ofisi ya waziri mkuu ni mali ya chama hivyo inapaswa itumie nembo ya chama? Na kuzungumzia uchaguzi wa Chadema siyo kosa, labda yeye Sumaye kaamua atoe maoni kama waziri mkuu mstaafu na siyo kama mwanachadema na ndio maana katumia nembo ya taifa.
hawa jamaa hawafai hata kupewa kijiji kuongoza
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimeshtushwa kuona mwanachama wake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akitumia nembo ya taifa katika barua yake ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika leo katika jengo la LAPF, lililopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa chama hicho hakina taarifa za mkutano huo na kwamba wameona barua hiyo mitandaoni kama ilivyokuwa kwa wananchi wengine.

Tunaona barua hiyo katika mitandao kama wengine, tumeshtushwa kuona barua yenye nembo ya Taifa inatumika kuitisha mkutano wa kiongozi wetu.

Sumaye anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari leo, mkutano ambao umeitishwa siku chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, ambapo licha ya kuwa mgombea pekee, alipata kura 48 za hapana kati ya kura 76 zilizopigwa.

Watu wakiendelea kujiuliza kiongozi huyo atazungumza nini, barua ya kuitisha mkutano huo imeeleza kuwa lengo la mkutano huo ni kuzungumzia masuala ya siasa nchini na mwenendo wa uchaguzi wa CHADEMA unaoendelea.

Amekuwa mwanachama wa CHADEMA kwa zaidi ya miaka minne sasa, ambapo alijiunga Agosti 2015 wakati wa harakati cha uchaguzi mkuu.

Kiongozi huyo pia amechukua fomu ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa, huku akisema kuwa lengo la kuchukua fomu hiyo ni kuuonesha ulimwengu kuwa ndani ya CHADEMA kuna Demokrasia, na sio kweli kwamba nafasi ya mwenyekiti haiguswi.

Chanzo: Swahili Times
Tunasubiri mvua za matusi ya kizaramo kutoka chama cha demokrasia na maendeleo ya misukule
 
Mtu kura zinashindwa kutosha kupitia sanduku la kura then eti mtu anakasirika anahama chama!

Ujinga ulioje?

Nilidhani ataonesha ma-evidence ya ya hizo figisu labda picha na videos na sound clips kudhibitisha aliibiwa kura kumbe mtu anaishia kuleta habari za kuhisi!

Sumaye is better than this nonsense!

Yaani mtu unadhani kwenye uchaguzi ni lazima uchaguliwe wewe tu!
 
Bado sana kuwa na watu makini kwenye siasa. Lowasa katusaliti, sasa Sumaye apewe uenyekiti tena!! wale wakimbizi wa kisiasa siwaamini katu, Mbowe usiachie ccm kina mtandao mrefu, kinarudi kinyumenyume kupenyeza mamruki kuweni makini. Wale wakimbizi wote hakikisha hawapewi nafasi ili kuua vyama vya upinzani please!
 
Ni wakati muafaka kwa sumaye kumpigia magoti JPM ili arudishiwe mapori yake yaliyo taifishwa !
 
Chadema hakina maana tena, chama hakiko tayari kuchukua dola, magufuli wacha awanyooshe shenzi kabisa.
 
Nafikri ifike mahali serikali ikubali wazo la mgombea binafsi,, hivi vyama vimezidi ujinga bora mtu uongozwe na mkeo!
Kwa hiyo, naye Sumaye angegombea UENYEKITI CHADEMA TAIFA, kama MGOMBEA BINAFSI?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kimeshtushwa kuona mwanachama wake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akitumia nembo ya taifa katika barua yake ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika leo katika jengo la LAPF, lililopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kuwa chama hicho hakina taarifa za mkutano huo na kwamba wameona barua hiyo mitandaoni kama ilivyokuwa kwa wananchi wengine.

Tunaona barua hiyo katika mitandao kama wengine, tumeshtushwa kuona barua yenye nembo ya Taifa inatumika kuitisha mkutano wa kiongozi wetu.

Sumaye anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari leo, mkutano ambao umeitishwa siku chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, ambapo licha ya kuwa mgombea pekee, alipata kura 48 za hapana kati ya kura 76 zilizopigwa.

Watu wakiendelea kujiuliza kiongozi huyo atazungumza nini, barua ya kuitisha mkutano huo imeeleza kuwa lengo la mkutano huo ni kuzungumzia masuala ya siasa nchini na mwenendo wa uchaguzi wa CHADEMA unaoendelea.

Amekuwa mwanachama wa CHADEMA kwa zaidi ya miaka minne sasa, ambapo alijiunga Agosti 2015 wakati wa harakati cha uchaguzi mkuu.

Kiongozi huyo pia amechukua fomu ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa, huku akisema kuwa lengo la kuchukua fomu hiyo ni kuuonesha ulimwengu kuwa ndani ya CHADEMA kuna Demokrasia, na sio kweli kwamba nafasi ya mwenyekiti haiguswi.

Chanzo: Swahili Times
alitumia nembo ya serikali kwa sababu alitumwa na serikali kwa kazi maalum iliyomshinda
 
Badala mshtushwe na uhuni wa Mwenyekiti asiye na mbadala?
 
Attachments

  • 78701338_445149639518457_3423827531984353425_n.mp4
    2.6 MB
Chukulia hapo ndio mtu keshapewa uenyekiti wa taifa alafu anaitisha press kjitoa chamani!
Cdm wamerisk katika hili lakini ni calculated risk na huenda 'ikawalipa' badala wa kuwagharimu. Time will tell
Na hili lingetokea tu kwa hali ya sasa. Anyway hawa walishatoa mchango wao kwenye taifa wakijitoa ni faida zaidi. Yanatakiwa mawazo mapya sana kwa kizazi chetu, dunia inakwenda kasi sana.
 
Kwa hiyo, naye Sumaye angegombea UENYEKITI CHADEMA TAIFA, kama MGOMBEA BINAFSI?
Gamujage nokho nyanda! Unafikri watu kutapatapa kote unafikri wanatafuta nini kama siyo kugombea nafasi? Mimi sikumaanisha kwenye vyama!
 
Back
Top Bottom