WALOLA VUNZYA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 7,154
- 7,155
Tumewaachia ili mnenepe
Msusie msisusie, mfoke msifoke, mlie msilie, mnune msinue, mbweke msibweke, haiwasaidii kitu maana kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Wabunge watapatikana tuu hata wote wakitoka CCM. Nyinyi mtabaki kufoka tu wenzenu wanacheka na nyavu! Kama baadhi ya vyama vimeshakubali kushiriki, CHADOMO ni mdudu gani mbele ya umma wa kitanzania! Leo watasema hawashiriki, kesho utashangaa wanakinga bakuli la njaa ya ruzuku! Hawa ni njaa tupu sasa hivi, hawana mbele wala nyuma wala kushoto wala kulia!